Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all 565 articles
Browse latest View live

Hat-trick yampaisha Hilika Zanzabar

$
0
0

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’,  Zanzibar

Mshambuliaji wa Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika jana amekuwa kinara kwa kucheka na nyavu baada ya kupiga Hat-trick timu yake iliposhinda 8-0 dhidi ya Kimbunga katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa katika dimba la Amaan.

Hat-trick hiyo imemfanya aongoze kwa kufunga mabao baada ya kufikisha mabao 11 akifuatiwa na mwenzake wa Zimamoto Hakim Khamis ‘Men’ mwenye mabao 10 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mudrik Muhib wa KMKM pamoja na Rashid Abdallah ‘Gaska’ wa Mafunzo ambao wote wana mabao 8 kila mmoja.

Msimu ulopita Hilika pia alipiga Hat trick katika hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar ambapo Zimamoto iliposhinda 6-0 dhidi ya Afrika Kivumbi mchezo uliopigwa katika dimba la FFU Finya huko Kisiwani Pemba.

Jumla ya Hat trick 4 mpaka sasa zimeshafungwa katika ligi hiyo ambapo alianza mshambuliaji wa zamani wa Jang’ombe Boys Abrahman Othman ‘Chinga’ ambaye kwasasa anacheza Singida United ligi daraja la kwanza Tanzania bara, na Hat trick ya pili ikafungwa na Khamis Maulid wa Polisi, ya tatu ikapigwa na Mshambuliaji wa timu ya Kipanga David Julius Nyerere ‘Chope’ na ya nne ndio hiyo ilopigwa na Hilika.


Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Himid Mao ‘Ninja’ wa Azam FC

$
0
0

Na Zainabu Rajabu

MAISHA ya mpira huenda kasi sana, dakika 90 pekee huweza kumfanya mchezaji awe mfalme au mtumwa katika timu. Shangwe na nderemo zinazozizima uwanjani kutokana na mapigo ya mpira kuwafurahisha wapenzi wa timu fulani, huenda sambamba na kipaji alichonacho mchezaji. Unapozungumzia mafanikio ya Azam FC, wapo wengi ambao huweza kutajwa.

Shuti  la mita 35 lilitosha kuhitimisha ndoto za wanasimba juu ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi wiki chache zilizopita visiwani Zanzibar. Aliyekatisha ndoto hizo ni kiungo Himid Mao ‘Ninja’ ambaye ndiye aliyekuwa shujaa kwa timu yake na kuipa ushindi timu ya Azam, mtandao wa shaffihdauda.co.tz   umemtafuta kiungo huyo na kuzungumza nae ambapo hapa antiririka kama ifuatavyo.

Historia yake.

Himid ni wa kwanza kuzaliwa katika familia yenye watoto watano. Ndugu zake wengine ni Femina, Rozmana, Faisal na Rahim.

Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Kiwandani, Turiani, Morogoro darasa la kwanza na la pili na kuhamia Karume ya Dar es Salaam na alisoma hadi darasa la sita. Alihama tena na kumalizia elimu ya msingi Shule ya Msingi ya Dk. Omary Ali Juma iliyopo Magomeni, Dar es Salaam kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Tabata ambako alimaliza kidato cha nne mwaka 2011.

Himid Mao ni mtoto wa nyota wa soka wa zamani, Mao Mkami ‘Ball Dancer’ aliyewahi kuwa mchezaji wa Pamba ya Mwanza, Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro na Moro United ya Morogoro.

Wadau wa soka wanakumbuka ‘Ball Dancer’, ambaye alipewa jina hilo na mtangazaji maarufu wa zamani wa Redio Tanzania, Charles Hillary.

Himid anafuata nyayo za baba yake kutokana na umahiri wake katika sehemu ya kiungo lakini kikubwa zaidi ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja.

Jina lake lilikuwa ni miongoni mwa wanasoka waliofanya  vizuri kwenye ulimwengu wa soka kwani alikuwa tegemeo kwenye timu za taifa za vijana wa chini ya miaka 17, 20 na 23.

Mtazamo wa Himid kuhusu chipukizi kwenye soka la kisasa

“Chipukizi wazuri na wana msaada kwetu, ukimuangalia Masoud Abdallah amekuwa anafanya vizuri kuliko wachezaji wote wa timu B amekuwa na msimu  mzuri,”

Vipi kuhusu kocha wake Iddi Cheche?

“Ni mtu mzuri ambae tumemzoea kama baba yetu ambae anatushauri mambo mengi sana kuhusu maisha pamoja na mpira unavyoendele katika karne hii”.

Bao lake bora kuwahi kufunga

“Bao bora nililowahi kufunga hadi sasa lilikuwa dhidi ya  Ruvu Shooting lilioisaidia timu yangu kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara”.

Nje ya soka Himid anapenda nini?

“Napendelea kulala na kucheza game (play station)”.

Kuhusu misosi je?

“Mimi sichagui wala sijivungi chakula, chochote  kinachokuja mbele yangu nakula”.

Umeoa?

“Nimeoa mke wangu anaitwa Hannan Abdulhafidh na tumebahatika kupata mtoto moja wa kike jina lake Balqis”

Rangi anazopenda Himid

“Nyeusi, Nyekundu, Nyeupe”

Unamiliki simu ya aina gani?

“iphone 6S”

Post za mastaa baada ya Simba kuifunga Yanga 2-1

$
0
0

Hakuna ubishi kwamba mechi ya Simba na Yanga inawaleta pamoja watu wa kada mbalimbali bila kujali vyama vyao vya siasa, dini, kabila wala rangi zao, wadau wa mchezo wa soka hujumuika kwa pamoja kushuhudia game hiyo maarufu zaidi kwenye mchezo wa soka Tanzania huku kila mmoja akiwa katika upande wake wa ushabiki.

Mechi ya Simba vs Yanga iliyochezwa Februaey 25, 2017 iliwaleta pamoja watu wengi pale uwanjani kuanzia wanasiasa, mastaa wa muziki wa Bongofleva, Bongo Movies na wengine kibao ambao ni wana majina makubwa Bongo.

Baada ya mechi hiyo kama ilivyo kawaida katika kizazi hiki cha digital, kila mtu akaonesha hisia zake kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram. Shaffihdauda.co.tz imefanikiwa kupata posts kadhaa za mastaa mbalimbali hapa Bongo wakitoa hisia zao kufatia ushindi wa Simba 2-1 Yanga huku wengine wakitupia post nyingine kutokana na namna tu game hiyo ilivyowakutanisha pamoja.

Haji S. Manara – Afisa habari Simba SC

Professor Jay – Mbunge/Msanii wa Bongofleva 

Ommy Dimpoz – Msanii Bongofleva

Jerry Muro – Afisa habari Yanga (amefungiwa) 

Mwana FA – Mwanamuziki Bongofleva 

Ridhiwani Kikwete – Mbunge

Mwigulu Nchemba – Waziri

Zitto Kabwe – Mbunge

Lulu – Mwigizaji Bongo Movies

Afande Sele – Mwanamuziki Bongofleva 

Yanga yalalamika Simba inabebwa

$
0
0

Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake wamelalamikia kutokuwepo na usawa kwa Simba na yanga katika matumizi ya viwanja vya Uhuru na ule wa Taifa.

Mkwasa amesema, Yanga kesho inatakiwa kucheza kwenye uwanja wa Uhuru mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga wakati Simba wao watatumia uwanja wa taifa siku ya Alhamisi kwenye mechi yao ya ligi kuu dhidi ya Singida United hivyo amesisitiza kuwepo na usawa kati ya vilabu hivyo juu ya matumizi ya viwanja tajwa.

Kuna wakati bodi ya ligi ilitangaza kuwa, Simba na Yanga zitatakiwa kucheza mechi zao kwenye uwanja wa Azam Complex kupisha shughuli za kiserikali siku ambazo timu hizo zingeutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao, badala yake yanga ilicheza azam complex mchezo wake dhidi Tanzania Prisons lakini mechi ya Simba ikachezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

“Tunatambua kwamba uwanja wa Taifa ulikuwa katika matengenezo na haujatumika kwa muda mrefu lakini kwa sasa unaonekana umekamilika, tulijaribu kuomba tuweze kuutumia lakini tumekosa hiyo fursa na tumepata taarifa kwamba kuna baadhi ya mechi zitachezwa poale lakini sisi mechi yetu ya kesho (Jumatano) itachezwa uwanja wa Uhuru.”

“Tulitegemea tungeanza kucheza pale lakini tunakosa hiyo fursa sasa inatupa shida upande wetu tunaonekana kama hatupewi thamani au umuhimu.”

“Nakumbuka mechi yetu na Prisons yanga ilicheza Jumamosi, Simba wakacheza Jumapili lakini sisi tukacheza kwenye uwanja wa Azam Complex  Simba wakacheza uwanja wa Uhuru kwa hiyo sisi tukakosa hiyo fursa, hii ni mara ya pili inakuwa wenzetu wanaanza kucheza na Singida Alhamisi kwenye uwanja wa taifa sisi kesho tumeambiwa tunacheza uwanja wa Uhuru.”

“Sasa angalieni namna gani hakuna usawa katika mambo kama haya, sisi tunaomba kuwepo na usawa kwa sababu hizi timu zote ni za watanzania wazalendo, kama kuna haki basi itolewe kwa sawa kwa vilabu vyote kuliko kubagua kwamba timu hii inatumia uwanja fulani hii inakosa fursa.”

Wababe wa Simba waishia mikononi mwa Singida Utd

$
0
0

Disemba 22, 2017 Simba ikiwa bingwa mtetezi wa kombe la shirikisho Tanzania bara ilivuliwa ubingwa na Green Warriors kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya sate ya kufungana 1-1 ndani ya dakika 90 ikiwa ni raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Sasa bwana leo Januari 31, 2018 kilichoipata Simba kimewarudia wababe wao Green Warriors ambao wametupwa nje ya mashindano hayo kwa penati 4-3 na Singida United baada ya timu hizo kutoka suluhu.

Kila timu na kibonde wake

  • Simba ilianza kupoteza game yake ya FA Cup dhidi ya Green Warriors inayoshiriki ligi daraja la pili japokuwa watu hawakuamini kama Warriors wangeweza kuangusha mbuyu.
  • Singida United ikiwa kati ubora wake baada ya kufanya makubwa kwenye kombe la Mapinduzi  ikakumbana na kipigo kikali cha magoli 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
  • Warriors wamepoteza nafasi kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kufungwa kwa penati na Singida United.

Matokeo ya mechi zote za leo kombe la shirikisho Tanzania bara.

Costal Union imerejea VPL, kocha kaweka historia baada ya miaka 30

$
0
0

Hatimaye Costal Union ya Tanga imefanikiwa kurejea ligi kuu Tanzania bara kwa ajili ya msimu ujao (2018/19) baada ya kupata matokeo ya ushindi wa magoli 2-0 dhiodi ya Mawenzi market ya Morogoro kwenye mchezo wa kundi b ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kocha mkuu wa Costal Union juma mgunda na msaidizi wake Joseph Lazaro wameandika rekodi ya aina yake kwa kuwa ndio wachezaji walioipa ubingwa timu hiyo miaka 30 iliyopita wakiwa wachezaji leo wakiwa makocha wanaiwezesha kupand daraja kucheza ligi kuu.

“Mwaka 1988 mimi na msaidizi wangu Joseph Lazaro tulikuwa wachezaji wa Costal Union tulioipa ubingwa Coastal Union mwaka huo, leo mimi tena nikiwa na mwenzangu yuleyule (Joseph Lazaro) baada ya miaka 30 tunatengeneza historia nyingine. Ni jambo linalonifurahisha sana na litachukua muda mrefu kufutika kwenye kumbukumbu zangu,” Juma Mgunda.

“Umati wa mashabiki uliokuja leo uwanja wa Jamhuri Morogoro kuishangilia timu yao ili ipande daraja, unanikumbusha enzi zetu wakati tunacheza tunapata support kubwa kutoka kwa mashabiki kama hivi, ni jambo la kufurahisha linalonikumbusha mbali na kunijengea historia nyingine kwenye timu ya Coastal Union.”

Magoli ya Coastal Union katika mchezo huo yamefungwa na Raidhin Hafidh na mkongwe Athumani Idd ‘Chuji’ nyota wa zamani wa polisi Dodoma, Simba, Yanga, Mwadui pamoja na timu ya taifa ya tanzania ‘Taifa Stars’.

Kutoka Kundi B Costal na KMC zimefuzu kucheza ligi kuu Tanzania bara zikiungana na JKT Tanzania.

Chuji kaweka mezani faili la Coastal kupanda daraja

$
0
0

Kiungo mkomgwe wa soka nchini Athumani Idd ‘Chuji’  amesema mechi za ligi daraja la kwanza ni ngumu na kuzifananisha na fainali. Chuji ameisaidia Coastal Union kurejea ligi kuu baada ya timu hiyo kushuka misimu miwili iliyopita.

“Tulichokuwa tunakitafuta leo tumekipata, tumefanya maandalizi tangu ligi inaanza leo tumefanikisha lengo ambalo tulikuwa tunalihangaikia, michezo ni migumu ukiangalia ligi daraja la kwanza kila mechi ni fainali.”

Chuji ambaye alifunga goli la pili kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B wakati Costal ikicheza dhidi ya Mawenzi Market na kushinda 2-0 ushindi ulioifanya irejee ligi kuu amekiri uzoefu wa baadhi ya wachezaji akiwepo yeye mwenyewe pamoja na Husein Sharif ‘Cassilas’.

”Sisi tuna wachezaji wengi wazoefu kwa hiyo tukiwaelekeza vijana wanaelewa kwa hiyo kwa pamoja tukitia nguvu matokeo yake ndio kama haya.”

“Timu inatakiwa ijipange iangalie iliteleza wapi ifanye marekebisho ili timu ifanye vizuri. Wanatanga wanatakiwa kuipenda timu yao na kuwa kitu kimoja ili kufanikisha malengo ya timu.”

Ukiachana na kuipandisha Coastal Union kucheza vpl msimu ujao, Chuji pia aliisaidia Mwadui kupanda ligi kuu akiwa nahodha wa timu hiyo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

KMC kufanyiwa party kusherekea ligi kuu

$
0
0

Baada ya kusubiri kwa takribani miaka miwili hatimaye timu ya manispaa ya kinondoni kmc leo imefanikiwa kupanda ligi kuu tanzania bara baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya JKT Mlale kwenye uwanja wa majimaji, Songea.

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo abdulhalim humoud dakika ya 45 kipindi cha kwanza lililodumu hadi dakika ya mwisho.

Kocha wa KMC Fred Felix Minziro ndiyo shujaa kwa upande wa timu hiyo ambaye pia aliisadia Singida United kupanda VPL msimu uliopita.

“Nawashuru viongozi wetu kwa kututia hamasa hususan katika mechi hizi tatu za mwisho ambazo tulijiwekea malengo ya kushinda zote ili tuweze kuingia ligi kuu, hamasa waliyotupa viongozi wetu ndiyo imefanya wachezaji wetu kujituma kwa nguvu sana.”

Tumezoea kumuona mwasyika akicheza kama mlinzi wa kushoto lakini katika mechi mbili za mwisho minziro amemtumia kama mshambuliaji.

“Eneo la ushambuliaji halikuwa vizuri sana hasa katika mechi kadhaa zilizopita walikuwa wakikosa magoli mengi kwa hiyo niliamua kumtumia mwasyika na ameleta tija ndani ya timu,” Minziro.

Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta ameongozana na timu hadi mkoani Ruvuma lakini pia amekuwa karibu na timu kwa baadhi ya mechi za mwisho.

“Tumetumia nguvu kubwa sana kumpata kocha Minziro yote ilikuwa ni kuhakikisha kwamba mwaka huu timu inapanda kucheza ligi kuu. Kama mnavyojua mwaka jana timu hii iliongoza hadi dakika za mwisho haikufanikiwa, mwaka juzi vilevile kwa hiyo mwaka huu nikiwa Mayor nikaamua kwenda na wachezaji bega kwa bega,” Benjamini Sitta.


Dar yachekelea ‘utitiri’ wa timu VPL

$
0
0

Uongozi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA ) chini ya mwenyekiti wake Almasi Kasongo unasherekea timu zake kuendelea kupanda ligi kuu tanzania bara baada ya JKT Tanzania na KMC kujihakikishia kucheza vpl msimu ujao huku wakisuri timu moja kati ya Friends Rangers au African Lyon ambazo mojawapo itaungana na nyingine mbili kucheza ligi kuu.

Timu hizo zitafanya Dar kuwa ndio mkoa wenye timu nyingi ligi kuu ambapo mkoa huo utakuwa na timu sita (Yanga, Simba, Azam, JKT Tanzania na KMC).

Kasongo amesema, walikubalina msimu huu wa ligi daraja la kwanza Dar ipandishe timu zisizopungua tatu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

“Kikubwa kilichonisukuma kuja Songea ni makubaliano yetu na timu zetu za Dar es Salaam, tulikubaliana kwamba mwaka huu tupandishe timu tatu na bahati nzuri uongozi wa DRFA uliweza kuzitembelea timu zote na tukakubaliana, sasa nimefarijika kuona mazungumzo yetu ya awali yanakamilika Songea kwa hiyo nikaona niwe sehemu ya ukamilifu wa jambo hilo.”

“Tunawapongeza vijana wamepambana na msimu ujao watacheza ligi kuu, KMC wamejitoa sana lakini nazipongeza pia timu nyingine za Dar ambazo zimetuwakilisha vizuri ikiwemo JKT Tanzania lakini pia kuna timu zetu mbili Friends Rangers na African Lyon ambazo zinasubiri kwenye foleni kunda ligi kuu.”

“Ukicheza Simba, Yanga, ukaondoka wanasahau bado ni mchezaji mzuri”-Humud

$
0
0

Watu wengi wamekuwa wakitafsiri mchezaji aliyefanikiwa kucheza ligi kuu anaporudi ligi daraja la kwanza biashara yake inakuwa imekwisha, lakini kiungo mkongwe Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ hakubaliani kabisa na jambo hilo na bado anaamini yuko fit kushindana na wachezaji wengine wa VPL.

“Mpira wa kibongo una mambo mengi hasa kwetu sisi wachezaji wazoefu ambao tumeshapita kwenye vilabu vikubwa, mpira wa tanzania ukishacheza simba na yanga ukiondoka watu wanasahau kwamba wewe bado ni mchezaji mzuri lakini vilabu hivyo vinahitaji kuwa na wachezaji wengine wapya hicho ndio wanasahau,” Abulhalim Humud.

“Kile ambacho kilinifanya nije kmc leo nimeweza kukitimiza pamoja na wachezaji wenzangu na tumeifikisha pale ambapo wanakinondoni wanataka iwepo.”

“Kizuri zaidi mpira ni mchezo wa hadharani sio kujificha kile ambacho kimefanyika au ambacho nakifanya tangu nimekuwa kmc kinatosha kuwa majibu kwa watu ambao walikuwa wanafikiria tofauti.”

Humud alifunga goli pekee lililoipandisha daraja KMC kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B walipocheza dhidi ya JKT Mlale kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Mdogomdogo Morocco wanatoboa Afrika

$
0
0

Michuano inayoshirikisha wachezaji wanao cheza ligi za nfani-Afrika (CHAN) imemalizika jana Februari 4, 2018 huku wenyeji Morocco wakiibuka mabingwa baada ya ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa fainali.

Mshindi wa tatu ni Sudan ambao waliifunga Libya kwa penati 4-2 baada ya kushuhudia dakika 90 zikimalizika huku timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Baada ya Morocco kufanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika wa michuano ya CHAN, hiyo ni ishara kwamba soka la nchini humo linakua kwa haraka siku za karibuni kutokana na mafanikio waliyoyapata katika kazi ya vilabu hadi taifa.

Morocco ndio mabingwa wa CHAN (wachezaji wanaocheza ligi za ndani-Afrika), ukienda upande wa vilabu barani Afrika Wydad Casablanca ya Morocco ndio mabingwa wa Caf Champions League.

Jambo jingine kubwa kuhusu Morocco ni kwamba taifa hilo limefanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Kwa hiyo Morocco kwa sasa kuna maendeleo makubwa ya soka, ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri barani Afrika.

African Lyon yakamilisha hesabu ligi daraja la kwanza

$
0
0

African Lyon imekamilisha idadi ya timu sita zilizopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kiluvya United katika mchezo wa mwisho wa Kundi A ligi daraja la kwanza.

Lyon ilikuwa inawania nafasi hiyo na Friends Rangers huku kila timu ikiwa na afasi ya kupanda ligi kuu kabla ya mechi hiyo. Rangers ilikuwa ikihitaji ushindi lakini ili ipande dataja ilibidi Lyon watoke sare au kupoteza mechi yao dhidi ya Kiluvya.

Licha ya Rangers kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mvuvumwa, bado matokeo hayo hayakuwasaidia kutokana na ushindi wa Lyon.

Matokeo ya mechi zote za leo Februari 5, 2018 Kundi A ligi daraja la kwanza

  • Kiluvya United 0-1 African Lyon
  • Friend Rangers 3-1 Mvuvumwa
  • JKT Tanzania 3-0 Mshikamano
  • Ashanti United 3-2 Mgambo JKT

Lyon inaungana na JKT Tanzania ambayo ilishapanda ligi kuu kabla ya mechi za mwisho za Kundi A.

Timu zilizopanda ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza ni African Lyon (Dar es Salaam), JKT Tanzania (Dar es Salaam), KMC (Dar es Salaam), Alliance Schools (Mwanza) Biashara United (Mara) na Coastal Union (Tanga).

KMC, Biashara United na Alliance Schools ni timu tatu ambazo ngeni ligi kuu (zitacheza kwa mara ya kwanza) huku nyingine tatu (JKT Tanzania, Costal Union na African Lyon zenyewe zikirejea ligi kuu kwa mara nyingine tena.

Tumeziona timu zilizopanda VPL msimu ujao, bingwa nani? Hii ndiyo njia mbadala

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

TIMU Sita ambazo zimefanikiwa kupanda ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao kutoka ligi daraja la kwanza tayari zimefahamika baada ya kukamilika kwa michezo ya Kundi A Jumatatu hii. JKT Tanzania, African Lyon, na Coastal Union zimerejea tena ligi ya juu, Biashara United, Alliance Schools Academy na KMC zikipanda kwa mara ya kwanza.

Kupanda kwa timu hizi ni mafanikio makubwa kwao, lakini kwa hakika ligi hiyo imekuwa ikiendeshwa vibaya mno, huku TFF na wasimamizi Bodi ya ligi wakishindwa kufanya jitihada za kuiboresha. Ukiachana na malalamiko mengi kuhusu waamuzi na uchezeshaji wao uliodaiwa kuzipendelea zaidi timu za nyumbani-sijui ni zipi kwa maana kila timu ilikuwa ikilalamika inapocheza ugenini-TFF imeshindwa kutatua tatizo hilo.

Sawa, timu hizo zimepanda lakini nani bingwa wa ligi hiyo? Ni aibu kwa ligi kubwa nchini kama hiyo kukosa bingwa wakati hata ligi za mitaani huwa zinatoa mshindi wa jumla katika michuano husika. Kushindwa kupatikana kwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa pili mfululizo ni ‘udhaifu’ ambao unapaswa kutatuliwa haraka na pia bingwa wa FDL hapaswi kupatikana kwa namna ambayo alipatikana bingwa wa mwisho-Mwadui FC msimu wa 2014/15.

Njia mbadala

Nimekuwa nikifuatilia ligi mbalimbali za barani Ulaya-zile za juu na za chini pia na huko nimekuwa nikivutiwa na namna vyama/mashirikisho ya soka ya maeneo husika yanavyopambana kila uchao kuhakikisha ligi zao zinachezwa kwa ushindani. Ushindani ndiyo msingi wa kutengeneza ubora katika mashindano husika na katika hili kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kutazamwa. Mfano, kwa takwimu zilizotoka mwezi uliopita, ligi daraja la kwanza England-Championship imekuwa minongoni mwa ligi tatu bora zinazotazamwa zaidi duniani. Inafuatiliwa zaidi ya La Liga-ligi ambayo imekuwa ikiwatoa washindi wa mataji ya Ulaya mwaka hadi mwaka katika misimu ya karibuni.

Championship iko juu ya La Liga ligi ambayo imetoa washindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mara 16 katika karne hii. Ushindani uliopo katika ligi hiyo unavutia sana. Kwanza kuna timu 24-baada ya kila timu kucheza michezo 46-mbili za juu zinapanda ligi kuu moja kwa moja huku kiongozi wa ligi akitwaa ubingwa. Kuanzia timu iliyomaliza nafasi ya tatu hadi ile ya sita zitacheza michezo ya ‘play off-nusu fainali’ nyumbani na ugenini, washindi wanakutana fainali na mshindi anapanda daraja kukamilisha timu ya tatu baada ya zile mbili za mwanzo.

Ili kuongeza ushindani hadi mwishoni mwa msimu-kuanzia nafasi za juu hadi chini ya msimamo-timu ya mwisho katika zile tatu zinazopaswa kushuka daraja la pili haitashuka moja kwa moja bali itacheza na mshindi wa play off kutoka ligi daraja la pili na anayeshinda anapanda.

Kama ile iliyopo Championship itashinda ‘play off’ dhidi ya timu ya tatu iliyotakiwa kupanda daraja la kwanza kutoka ligi daraja la pili basi haitashuka. Hii inaongeza ushindani kwa timu sita hadi nane ambazo za chini ya msimamo kwani zitakuwa zikiitolea macho hadi ile nafasi ya kucheza michezo ya play off na timu kutoka chini. Kama chini ya msimamo kunakuwa na ushindani wa timu nane-kuwania nafasi moja ya upendeleo ya kutoshuka.

Timu nane zinakuwa na nafasi ya kupigania kuingia sita bora, nane nyingine zinakuwa na nafasi ya kupigania kupanda ligi kuu moja kwa moja. Ujerumani, Italia, Romania, Poland, Ubelgiji, Ufaransa, Hispania, Holland, Hispania ni baadhi ya nchi ambazo utaratibu wake wa timu kupanda ligi ya juu zaidi unavutia na TFF kwa kushirikiana na bodi ya ligi wanaweza kutazama huko na kujifunza zaidi na baadae kutumia baadhi ya taratibu nzuri ambazo zitaupendezesha na kuuendeleza mchezo huu nchini.

Kwa vile ligi kuu ya Vodacom kuanzia msimu ujao itakuwa ikishirikisha timu 20 huku zikiwania nafasi moja tu ya ‘ubingwa’ ili kuiwakilisha nchi katika michuano ya Caf, TFF na Bodi ya ligi wanakabiliwa na changamoto kubwa kuhakikisha ushindani unakuwepo. Kama kutakuwa na timu nane ama kumi zenye uwezo wa kushindania taji tutapata ligi bora lakini kama zitaendelea kubaki Yanga, Simba na Azam FC ni wazi hakutakuwa na ligi bora bila kuumiza akili na kutafuta majawabu.

Ligi ya makundi imeshapitwa na wakati na timu ishirini kugombea nafasi moja tu yenye maana ni wazi si rahisi kupata ubora. Hivyo basi ni lazima waendeshaji wakae na wadhamini na kutazama namna ya kuboresha zawadi kwa kila nafasi katika msimamo wa ligi-kuanzia nafasi ya kwanza hadi ya 17.

Mfano, timu itakayomaliza nafasi ya 17 itapata milioni 30, itakayomaliza juu yake itapata kiasi cha juu zaidi hadi kufika kwa bingwa. Timu zitakazomaliza nafasi ya 20 na 19 zawadi yao ni kushuka dara, na ile itakayo maliza nafasi ya 18 ipewe nafasi ya upendeleo kucheza na timu ya tatu ambayo ilipaswa kupanda ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza. Hii itategemea pia na muundo wa ligi daraja la kwanza utakavyokuwa.

Hapa kunasaidia kuwepo na ushindani kwa timu nane chini ya msimamo, lakini pia kutaifanya FDL kuwa na ushindani zaidi na hivyo kutatengenezwa ubora unaotakiwa.

Kuzikataa timu za taasisi moja katika ligi moja

Katika ligi daraja la kwanza iliyomalizika Jumatatu hii kulikuwa na timu nane za Majeshi, timu mbili za taasisi na sita za uraiani. Kulikuwa na timu mbili za Jeshi la Polisi-Polisi Tanzania FC na Polisi Dar FC na bahati mbaya zote zilipangwa kundi moja. Kulikuwa na timu nne za Jeshi la kujenga Taifa (JKT)-JKT Tanzania, JKT Mgambo (zilipangwa kundi moja), JKT Mlale na JKT Oljoro, pia kulikuwa na timu mbili za jeshi la Wananchi-Rhino Rangers na Transit Camp (zilipangwa kundi moja) TFF haipaswi kukubali tena kuona timu za Taasisi moja zikicheza ligi moja.

Inapaswa kuwashinikiza wamiliki wa vilabu hivyo kufuata taratibu zinazokubalika katika uendeshaji wa soka la kisasa hivyo watafute haraka namna ya kuondoa mkanganyiko wa kuwa na timu zenye maslahi mamoja. Kuendelea kuwa na timu za Taasisi moja hakutaweza kutuletea maendeleo yanayotakiwa katika soka japo ni kweli Polisi Tanzania imeshindwa kupanda baada ya kuharibiwa na Polisi Dar iliyoshuka daraja katika mchezo ambao Polisi Tanzania waliondolewa kileleni na kushindwa kururejea tena mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi.

Isiwe makundi tena

Timu 16 zishindane katika mfumo wa ligi ya mzungo mrefu. Ligi ya makundi hasa kwa ligi muhimu kama daraja la kwanza imepitwa na wakati na kama timu haina uwezo wa kucheza ligi yenye michezo 30 timu hiyo haipaswi kucheza ligi kuu kwani haijiwezi na kama timu haijwezi kuwa nayo ligi kuu ni sawa na kubeba mzigo mzito usiojua unaupeleka wapi.

Hata kama si kwa mfumo nilioupendekeza, TFF na Bodi ya ligi wanapaswa kuhakikisha ligi ya msimu ujao inachezwa kwa mfumo wa ligi na si michuano kama ilivyo sasa. Michezo 14 kuipandisha timu ligi kuu ni michache mno na njia pekee ya kuepukana na hilo ni timu 16 kucheza pamoja zenyewe kwa zenyewe-nyumbani na ugenini.

Niyonzima kufanyiwa upasuaji India

$
0
0

Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima anatarajia kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu unaomsumbua na kumfanya asionekane uwanjani siku za karibuni kutokana na kuuguza majeraha.

Afisa habari wa Simba Haji Manara wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema, Niyonzima ataondoka nchini ndani ya siku mbili hizi kuelekea India kwa ajili ya matibabu.

“Haruna Niyonzima anatarajia kusafiri ndani ya siku hizi mbili kwenda India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu kutokana na maumivu yanayoendelea kumsumbua, haitachukua zaidi ya wiki mbili atakuwa amerejea uwanjani kwa sababu ni upasuaji mdogo tu”-Haji Manara, afisa habari Simba.

Niyonzima ambaye alisajiwa na Simba baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga hajaonekana uwanjani katika mechi kadhaa na imekua ikielezwa kwamba ni kutokana na majeraha.

Kuhusu wachezaji wengine waliokuwa wanasumbuliwa na majeraha ya mufa mrefu (Said Mohamed ‘Nduda’ na Salim Mbonde) Manara amesema nyota hao wapo tayari kuendelea na mazoezi ya pamoja na timu nzima.

“Wachezaji wengine wa Simba ambao walikuwa na majeraha wameanza kurejea kwenye mazoezi ya pamoja na timu. Said Mohamed ‘Nduda’ ameshaanza mazoezi lakini Salim Mbonde anatarajia kujiunga mazoezini wakati wowote kwa sababu ameshamaliza program ya gym na beach.”

Manara hataki Yanga wazomewe

$
0
0

Uongozi wa klabu ya Simba umewaomba mashabiki wake kutowazomea wachezaji wa Yanga watakapokuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya kombe la vilabu bingwa Afrika Jumamosi dhidi ya St. Louis Suns United kwenye uwanja wa taifa.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, hawana undugu na Yanga lakini mashabiki wa Simba wasiwazomee kwa sababu watakuwa wanawakilisha nchi.

“Nawaomba mashabiki wa Simba wasiende kuizomea Yanga kwenye mechi yao ya kimataifa siku ya Jumamosi, kama hawawezi wasiende uwanjani. Sisi sote ni wawakilishi wa nchi, tunapofungwa na timu kutoka nje hawasemi wameifunga Yanga au Simba wanasema wameifunga Tanzania”-Haji Manara.

“Yanga si maadui zetu, ni watani zetu, ‘kucharurana’ kubaki kwenye mechi zetu za hapa nyumbani, kama wao watatuzomea ni wao siwezi kuwaomba wasifanye hivyo.”

Manara amesema Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassani Mwinyi atakuwa mgeni rasmi kwenye mechi yao ya Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie Nationale siku ya Jumapili kwenye uwanja wa taifa.

Simba imetangaza viingolio kwa ajili ya mchezo huo ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa ni Tsh. 5000 kwa viti vya mzunguko.

Viingilio vingine katika mchezo huo ni VIP A Tsh. 30,000, VIP B Tsh. 20,000, viti vya Orange Tsh. 10,000.


Baada ya kupanda ligi kuu, KCM inarudishwa kwa wananchi Kinondoni

$
0
0

Baada ya kupanda daraja wiki moja iliyopita, timu ya KMC FC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni itatambulishwa rasmi kwa wanachi wa wila hiyo na mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla siku ya Jumamosi kwenye viwanja wa Biafra.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesema timu hiyo itapita mitaa mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni kabla ya kufika uwanjani kwa ajili ya kuitambulisha.

“Timu hii inapanda kwa mara ya kwanza ligi kuu Tanzania bara lakini ukiondoa vilabu vikubwa vya Simba na Yanga, timu hii ikiwa ni mali ya umma kwa maana taasisi ya kiserikali imeweka historia ya kuigwa sisi tungependa iwe mfano kwa taasisi nyingine kuinua vipaji lakini kupendezesha huu mchezo tunaoupenda katika jamii zetu”- Benjamini Sitta.

“Kwa hiyo tumeamua siku ya Jumamosi iwe siku ya kuipokea timu katika viwanja vya Biafra, saa sita timu itgaondoka ofisi za Manispaa ya Kinondoni na kupita mitaa mbalimbali halafu saa nane itakuwa uwanja wa Biafra ambapo tungependa kujumuika na wana Kinondoni wote lakini wana Dar es Salaam wote. Atakuwepo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, mkuu wa wila ya Kinondoni na viongozi mbalimbali.”

“Kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama Stamina, Roma, Madee na wasanii wengine wa Kisengeli ambao watahakikisha shughuli inapendeza. Tunafanya yote haya kwa ajili ya kuipongeza timu yetu.”

Simba kuna ‘presha’ kubwa”-Aishi Manula

$
0
0

Golikipa namba moja wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aishi Manula ameweka wazi tofauti iliyopo kati ya timu mbili ambazo amezitumikia hadi sasa (Azam na Simba) katika ligi kuu Tanzania bara kwa vipindi viwili tofauti.

Manula amabaye amekulia Azam amesema klabu ya Simba ina mashabiki wengi na kuna presha kubwa nyuma yake lakini pia kuna hamasa kubwa ukilinganisha na ilivyo kwa upande wa Azam ambayo ni timu changa inayoendelea kukua siku hadi siku.

“Tofauti iliyopo ni kwamba nipo sehemu ambayo ina mashabiki wengi zaidi, kuna presha kubwa zaidi kutoka kwa watu wanaoipenda hii timu  kwa hiyo hamasa ni kubwa zaidi kuliko nilikotoka.”

Manula ndiyo golikipa pekee wa VPL ambaye ameruhusu magoli machache kwenye ligi (amefungwa magoli sita) katika michezo 17 ambayo amesimama kwenye goli la Simba msimu huu. Amesema ubora wake pekeyake hautoshi kumfanya kuwa salama golini bali ushirikiano wa timu nzima ndio unamfanya anonekane imara langoni.

“Ushirikiano wa timu nzima ndio unanifanya niwe bora, hata golikipa uwe unaruka kama nyani huwezi kupambana kuzuia lile goli ambalo ni kubwa kuliko mimi kwa hiyo ni lazima tushirikiane wote kwa pamoja kama timu kuzuia magoli ndiyo maana hadi leo tumekuwa timu iliyoruhusu magoli machache. Ukiangalia tunapocheza mechi zetu mara nyingi mpira unaposimama tunazungumza timu nzima wapi kuna mapungufu na wapi tunafanya vizuri ili kufanya marekebisho tufikie malengo.”

“Kitu kingine ni mazoezi ambayo nafanya pia yanachangia nionekane bora, nipo chini ya kocha mzuri ambaye ana rekodi nzuri kiuchezaji kwa sababu alishaheza timu ya taifa na alicheza nje ya nchi (Msumbiji) kwa hiyo ni kocha ambaye anatufanya kuwa bora.”

Golikipa huyo anatarajia kusimama golini kwenye mchezo wa kimataifa (Caf Confederation Cup) kati ya Simba dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, mechi hiyo  licha kuwa ya kwanza kwa Simba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini kwa Manula ni mwendelezo wa kushiriki mashindano ya Afrika ngazi ya vilabu kwa sababu amefanya hivyo misimu kadhaa akiwa na Azam.

“Huu ni mwendelezo wa kile ambacho nilikuwa nakifanya awali kwa sababu nikiwa Azam kwa misimu mitatu au minne tulikuwa tunashiriki mashindano haya, sasa hivi nimebadili timu kwa hiyo kitu ambacho kipo akilini mwangu ni kuonesha utofauti kama mchezaji nahitaji kutengeneza profile yangu, wakati nikiwa Azam mara nyingi tulikuwa tukiishia hatua za mwanzo nataka kufika hatu nyingine mbele zaidi nikiwa na Simba.”

“Ukiangalia Simba ilishafika hatua kubwa zaidi kwenye mashindano ya kimataifa, sisi pia tunaliangalia hilo kama kipindi cha nyuma wenzetu waliweza kuifikisha mbali klabu yetu tunatakiwa kupigana kuvunja rekodi ambazo tayari zimewekwa na kutengeneza historia mpya kwa kufanya makubwa zaidi kuliko yaliyopo.”

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kuipa nguvu timu yao na wenyewe wanaona kama moto basi ndiyo umewaka, tuna kila sababu ya kushinda na nimeshasema tunataka kuweka historia kama wenzetu walivyoweza kuweka historia zao.”

Bocco amewaita mashabiki uwanja wa Taifa

$
0
0

Mshambulaji wa Simba John Bocco amewaomba mashabiki wa timu  kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuishuhudia timu yao ikicheza kwa mara ya kwanza mashindano ya Afrika baada ya kupita misimu mitano bila timu yao kushiriki mashindano hayo makubwa Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Bocco amesema mashabiki waoneshe hamu yao ya ku-miss michuano hiyo kwa kuishangilia Simba mwanzo-mwisho lakini wao kama wachezaji watahakikisha unapatikana ushindi mkubwa kwa ajili ya mashabiki na kupunguza mzigo wa mechi ya marudiano.

“Tumebeba dhamana ya mamilioni ya wapenzi wa Simba, naomba mashabiji waje kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao waoneshe hamu yao ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa kushangilia mwanzo mwisho, sisi tutapambana ili kupata ushindi mkubwa utakaoturahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano”-John Bocco, nahodha Simba.

“Wachezaji tunafikiria kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, ubora tuliouonesha kwenye ligi tunataka kuuhamishia kwenye mashindano ya afrika, itakuwa haina maana kama tutaishia kufanya vizuri kwenye ligi yetu.”

Leo Februari 11, 2018 Simba itacheza mchezo wa Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti ikiwa ni mchezo wa awali katika mashindano hayo ambayo mara ya mwisho Simba kushiri ilikuwa ni Mei 2012 Al Ahly Shendi ilipowatupa nje ya mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

Simba imerudi anga za kimataifa

$
0
0

Simba wamerejea kwenye anga za kimataifa kwa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Gendarmerie National ya Djibouti katika mchezo wa Caf Confederation Cup.

Wekundu wa Msimbazi wamesubiri kwa miaka mitano (5) mfululizo tangu waliposhiriki kwa mara ya mwisho mwaka 2012 na kuondolewa Al Ahly Shendi kwenye michuano ya vilabu bingwa Afrika.

Magoli ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa na Said Hamisi Ndemla, John Bocco ambaye amefunga magoli mawili huku goli la mwisho likifungwa na Emanuel Okwi.

  • Pacha ya ushambuliaji inayoundwa na John Bocco na Emanuel Okwi imeendeleza makali yake hadi kwenye michuano ya Afrika baada ya wawili hao kufunga magoli matatu kwa pamoja. (Bocco amefunga magoli mawili, Okwi amefunga goli moja na kumtengeneza goli moja lililofungwa na Bocco.

Video-Kocha Simba kawajibu wanaobeza 4G kimataifa

$
0
0

Baada ya Simba kushinda kwa magoli 4-0 kwenye mcheO wao wa kwanza wa kimataifa dhidi ya Gendarmerie, mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wanasema Simba ilikuwa na uwezo wa kupata ushindi mkubwa zaidi ya walioupata kutokana na udhaifu wa wapinzani wao.

Kocha msaidizi wa Sima Masoud Djuma amesema waliwataka wachezaji wasitumie nguvu kubwa kwenye mchezo mmoja kutokana na kukabiliwa na michezo miwili ya VPL hivi karibuni.

“Nimemsikia mwalimu wao anasema zamani walikuwa wanafungwa hadi magoli tisa au 10, huo ni mpira wa zamani, mpira wa kisasa kitu cha muhimu ni kwamba hatukuruhusu kufungwa goli.”

“Halafu sisi tuna mechi mbili za ligi zimeongozana hapa karibu kwa hiyo ilikuwa lazima tucheze kwa mpangilio kwa sababu ni lazima tushinde zote kwa hiyo hatukutumia nguvu nyingi kwenye mchezo mmoja.”

“Tunashukuru tulipata magoli ya mapema nafasi za kufunga zilipatikana lakini walikuwa wanacheza mchezo wa kukaa nyuma”

Viewing all 565 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>