Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all 565 articles
Browse latest View live

Azam inasubiri Simba, Yanga, fainali Mapinduzi Cup2017

$
0
0

dsc_0051

Club ya Azam FC imefuzu hatua ya fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa kuanzia saa 10:15 jioni

Frank Domayo ndiye mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo lililoivusha Azam na kuifanya icheze fainali na mshindi wa fainali ya pili kati ya Simba na Yanga itakayoanza saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

dsc_0038

Mbali na kuifungia timu yake bao la ushindi, Domayo alitangazwa Man of the Match kutokana na kiwango chake kuwa bora katika mchezo huo.

dsc_0816

Baada ya mchezo, Domayo alikabidhiwa kiatu cha kuchezea kama tuzo ya kuibuka mchezaji bora wa mechi lakini kama ilivyo utaratibu katika mashindano ya mwaka huu, alipatiwa crton nne za Malti kutoka kampuni ya Bakhresa.

dsc_0044


Yanga imetoneshwa kidonda, Simba vs Azam fainali Mapinduzi Cup2017

$
0
0

dsc_0288

Yanga imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika bila timu hizo kufungana.

Baada kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye michuano hiyo na kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa fainali ambao utachezwa siku ya Iajumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku moja baada ya kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar (January 12).

dsc_0291

Golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan kwenye changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya kwanza.

Penati nne za Simba zilifungwa na Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Boukungu.

Method Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’.

dsc_0265

Simon Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga penati zao huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji wao penati zao zilitua kwenye mikono ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.

dsc_0084

Video: Goli la Frank Domayo lililoipeleka Azam fainali Mapinduzi Cup2017

$
0
0

dsc_0062

January 10, 2017 ilichezwa michezo ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam FC ndio ilikuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya fainali ya Mapinduzi kufatia ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe mechi iliyotangualia mapema saa 10:15 jioni.

Frank Domayo akiwa katika ubora wake ndio aliwafungia Azam bao pekee lililowavusha na kuwapeleka hatua ya fainali baada ya miaka mitatu kupita.

Dawa ya Simba ipo tayari, bado kuwanywesha tu – Kocha Azam FC

$
0
0

screen-shot-2017-01-09-at-9-26-03-pm

Baada ya mishemishe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kesho Ijumaa January 13 ndio kilele cha kombe la Mapinduzi michuano ya 11 ambayo ilizinduliwa rasmi December 30.

Kuelekea mchezo wa huo utakaoshuhudia Azam na Simba zote zinazocheza ligi kuu Tanzania bara zikipambana, kocha wa muda wa Azam Idd Cheche amesema tayari anayo dawa ya Simba kilichobaki ni kuwanywesha.

“Kila timu na dawa yake, Simba dawa yao ipo wasubiri kunyweshwa,” anasema kocha wa muda Idd Cheche aliyeifikisha Azam hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup 2017 bila timu yake kuruhusu goli.

“Timu hizi mimi nazifahamu tangu nikiwa mchezaji, nimecheza nazo nikiwa mchezaji na sasa hivi ni mwalimu najua najua jinsi ya kuzikamata. Sisi tunazitaka timu zinazojiamini kwa sababu sisi tunajiamini zaidi yao.”

Mfumo

“Kuna plan mpya nakuja nayo mtaiona siwezi kuisema mapema lakini nitawashangaza watu uwanjani.”

Maingizo ya wachezaji wapya

“Hili bado ni la ndani kwanza, hatuwezi tukalisema hadharani kwa sababu hii ni sawa na vita kwa hiyo tunajipanga kimya-kimya wakija kustuka wanakuta shughuli inaendelea.”

Majeruhi

“Wachezaji wangu wote wako vizuri isipokuwa Hamisi Mcha ambaye ana matatizo kidogo.”

Dk. Shein ametaja mafanikio matatu ya michezo Zanzibar

$
0
0

Amaan Stadium

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’,  Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametaja mambo matatu makubwa katika Sekta ya Michezo kama mafanikio makubwa kwa mwaka uliopita wa 2016.

Mafanikio hayo ameyataja wakati  akizungumza  katika kilele  cha  maadhimisho  ya  sherehe  ya  miaka 53  ya  Mapinduzi  ya  Zanizbar  katika  uwanja  wa  Amani  hapa  kisiwani Unguja.

Amesema mambo makubwa katika Sekta ya Michezo katika Mwaka 2016 ni Bonanza la Taifa la mazoezi ya viungo, Vifaa vya michezo kugaiwa bure pamoja na Ujenzi wa viwanja vya kitogani na mpango wa kujenga viwanja vingine vitatu katika Mikoa mitatu tofauti.

“Katika sekta ya Michezo yale maadhimisho maalum ya siku ya mazoezi ya Viungo kitaifa yanofanyika kila mwaka tarehe 1 January nayo yameendelea kufanyika, vile vile Serikali imeendelea kutoa vifaa vya michezo kugaiwa bure kwa timu mbali mbali na imeanza kutekeleza agizo ya ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015-2020, ambapo kiwanja cha michezo kwa Wilaya ya Kusini Unguja kimeanza kujengwa kule Kitogani kati ya viwanja vitano vilivyoagizwa na ilani ya CCM na mpango wa kujenga viwanja vingine vitatu umeshaanza kutayarishwa katika Mikoa ya Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja na Mjini Magharibi”.

Maadhimisho  hayo  yalihudhuriwa  na  viongozi  mbalimbali  akiwemo  Makamu  wa  Raisi  wa  Jamuhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Mama  Samia  Suluhu  Hassan, Rais  mstaafu  wa  Tanzania  wa  awamu  ya  nne  Dk.  Jakaya  Mrisho  Kikwete, Waziri  Mkuu  wa  Jamuhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Kassim  Majaliwa,  viongozi  wa  kidini  na  kiserikali  kutoka  Tanzanaia  bara  na  visiwani Zanzibar.

Simba, Yanga, asanteni kwa kuja Zanzibar

$
0
0

IMG_0409

Hatimaye timu ya Azam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taji la Mapinduzi baada ya ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao safi la Himidi Mao akipasia nyavu kwa shuti kali akiwa nje ya box ndilo limeipa Azam kwa mara ya tatu wa kombe hilo.

Awali timu za Simba na Yanga zilipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na moto wao kwenye ligi kuu Tanzania bara huku Azam ikipewa nafasi ndogo kwa kuangalia rekodi zake kwenye ligi pamoja na kuondokewa na kocha wao siku za usoni.

Rekodi za Azam bada ya kuchukua ubingwa wa Mapinduzi 2017

  • Azam ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu goli hata moja kwenye mashindano ya mwaka 2017.
  • Ubingwa wa mwaka 2017 unaifanya Azam kuifikisha mataji matatu na Simba kwa idadi mataji ya Mapinduzi tangu mwa 2007. Azam imechukua taji hilo mwaka 2012, 2013 na 2017.
  • Azam imezifunga Simba na Yanga kabla ya kutwaa taji la Mapinduzi 2017 (Azam 4-0 Yanga mechi ya nusu fainali, Azam 1-0 Simba mchezo wa fainali)

Kuzifunga Simba na Yanga ni sawa na kukamata Kambale – Kocha Azam FC

$
0
0

20170107_221309

Baada yashinda kuiongoza Azam kushinda ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa kuifunga Simba 1-0 kwenye mechi ya fainali, kocha wa muda wa Azam FC Idd Cheche amesema, kuzifunga Simba na Yanga ni kama kumkamata Kambale (aina ya samaki).

Cheche anasema hivyo baada ya kufanikiwa kuvifunga vilabu hivyo vikongwa vya kwenye soka la Tanzania na kupata matokeo kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua makocha wengi nchini pindi wakutanapo na vilabu hivyo.

“Mshikamano na umoja wetu kwa sababu mimi timu zote nazijua, najua kila timu ipoje kwa hiyo ni kama vile unataka kumkamata Kambale, ukimshika kichwa basi hana ujanja,” anasema Cheche ambaye ameiongoza Azam katika mechi tano za Mapinduzi uku timu ikishinda mechi nne na kutoka suluhu mchezo mmoja.

Cheche hakuacha kuwapongeza wapinzani wake wa mchezo wa fainali kwa kusisitiza kuwa licha ya Azam kuibuka na ushndi lakini mchezo haukua rahisi kwao.

“Mchezo ulikuwa mgumu, nawapongeza Simba walijitahidi kutupa presha lakini mwisho wa siku tumeshinda.”

Omog amelivulia kofia goli la Himid Mao

$
0
0

20170114_080530

Ule ‘muwa’ uliopigwa na Himid Mao kuiandikia bao Azam dakika ya 13 kipindi cha kwanza hakua wa mchezo-mchezo kabisa.

Himid aliachia kombora kali ambalo golikipa wa Simba Daniel Agyey hakujua lilipita wapi kwenda nyuma ya nyavu zake.

Baada ya mechi kumalizika, Himid alikwenda kusalimiana na kocha wa Simba Joseph Omog ambaye alimfundisha kiungo huyu wakati walipokuwa pamoja Azam kabla ya Omog kutimuliwa ndani ya klabu hiyo.

Omog hakuacha kumpongeza Himid kwa aina ya goli aliloifunga Simba na kuipa Azam ubingwa wa tatu wa Mapinduzi Cup katika historia.

“Congratulations, it is a fantastic goal,” anasema Omog akionesha kulikubali bao la Himid ambaye aliwahi kumfundisha wakati alipokuwa kocha mkuu Azam FC na kufanikiwa kushinda taji la VPL mara ya kwanza msimu wa 2013-14.

Goli la Himid Mao lilikuwa la saba kwa Azam kwenye mashindano ya mwaka 2017 huku yenyewe ikiwa haijaruhusu goli hata moja hadi mwisho wa mashindano.


PICHA4: Nyuso za Simba baada ya kupoteza fainali Mapinduzi Cup 2017

$
0
0

IMG_0348

Hakuna timu inayopenda kupoteza mchezo hasa mechi ya fainali huku kombe likiwa limewekwa tayari kwa ajili ya bingwa.

IMG_0317

Hiki ndicho kimewatokea Simba usiku wa Ijumaa January 13 kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

IMG_0353

Wakiwa wanajua kabisa wakishinda mechi watakuwa mabingwa wapya na kukabidhiwa kombe la Mapinduzi 2017, Simba walijikuta wakiishia kuhuzunika kutokana na kupoteza mchezo wao wa fainali mbele ya Azam.

IMG_0366

Fairid Musa amefunga kwenye mechi yake ya kwanza Hispania

$
0
0

20170115_090401

Kijana Farid Musa ameanza vyema maisha yake ya soka nchini Hispania baada ya kufanikiwa kuifungia magoli mawili timu yake ya Tenerife B wakati akicheza mechi yake ya kwanza tangu awasili kwenye klabu hiyo.

Fairid alikuwa aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 wakati ikichuana na CF Unionviera.

Nyota huyo ambaye amesajiliwa kwa mkopo amepelekwa timu B kwa ajili ya kufundishwa baadhi ya mambo ikiwemo mfumo unaotumiwa na timu yake kabla ya kuanza kuingia kwenye timu ya kwanza.

Twite wa Yanga amesajiliwa timu moja na mchezaji wa Simba

$
0
0

20170115_090207

Kiraka wa zamani wa Yanga Mbuyu Twite pamoja na kiungo wa zamani wa Azam FC Michael Balou wamesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Fanja FC ya Oman.

Wote wawili walikuwa wakicheza ligi kuu Tanzania bara kabla ya kumaliza mikataba yao na kuondoka kufatia kutoongezewa mikataba mipya.

Baada ya kutua Fanja FC, wanaungana na mtanzania Danny Lyanga aliyepata kucheza Coastal Union na Simba SC.

Michael Balou anaungana na ndugu yake Kipre Tchetche waliyecheza pamoja Azam FC lakini Oman watakuwa timu tofauti. Balou akiwa Fanja FC, Tchetche yeye yupo Al Suwaiq.

Mtanzania kapata ushindi kwenye Marathon India

$
0
0

20170115_164632

Mtanzania Alphonce Simbu, amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mbio ndefu za Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akiwapiku Mkenya Joshua Kipkorir pamoja na wakimbiaji wengine wazoefu kutoka mabara mbalimbali.

Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai Marathon hufanyika Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji la Mumbai nchini India na yanaaminika kuwa ni mbio kubwa kabisa barani Asia kwa idadi ya washiriki wanaomaliza mbio.

Simbu, yupo chini ya 7udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania, aliibuka mshindi baada ya kutumia muda wa saa 2:09:28 muda ambao ni mzuri kwa mbio za aina hiyo.

Simbu amesema kuwa anaamini ushindi huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya.

Amesema ushindi huo kwake ni changamoto kwa mashindano mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesema ushindi huo siyo wake peke yake au wathamini wake , bali ni ushindi wa Taifa zima la Tanzania.

Kwa upande wa Serikali,  Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye amempongeza kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akisema , “Tumefanikiwa tena, hongera Simbu, hongera RT (Chama cha Riadha Tanzania), asanteni Multichoice Tanzania kwa kumsapoti. Mungu ibariki Tanzania.”

20170115_164546

Mkuu wa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema Multichoice imefurahi sana kwa matokeo huku akisisitiza kuendelea kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea taifa sifa kubwa.

“Tulichukua jukumu la kumdhamini Simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote.

Alisema Mshana na kuongeza “Dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudani”

Katika mbio hizo, waigizaji maarufu wa .Bollywood John Abraham and Neha Dhupia walikuwepo kuleta amsha amsha kwa washiriki.

Alphonce anatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatatu.

Klabu ya Oman imemnasa striker wa Simba

$
0
0

IMG_4521

Habari inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu kuondoka kwa mshambuliaji wa Simba Frederick Blagnon ambaye anaelekea kwenye klabu ya Oman Club ya nchini Muscut.

Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruha ya muda mrefu.

Story ya kuondoka kwa Blagnon imeanzia Instagram ambapo Haji Manara amepost picha ya Blagnon inayoambatana na maelezo kwamba nyota huyo anaondoka Simba kwenda Oman Club kwa mkopo wa miezi sita.

“Frederick Blagnon aenda kwa mkopo Oman Club ya Muscut kwa majariio ni mkopo wa miezi sita,” ni ujumbe aliouandika Haji Manara afisa habari wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

20170116_090057

Official: Okwi avunja mkataba na Sonderjyske Fodbold, Kurejea Msimbazi?

$
0
0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda,  Emmanuel Okwi ameachana rasmi na klabu ya  Sonderjyske Fodbold ya Denmark kwa makubaliano ya pande zote kuamua kusitisha mkataba. 
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Danish Superliga Jorgen Haysen uamuzi huo umefikiwa baada ya Okwi kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.

“Okwi hakuwa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi chetu, na matumaini ya kupata nafasi yamekuwa ya chini sana. Matokeo yake tumekubaliana kububja mkataba, tunamtakia kila la kheri huko mbeleni.’ 

Klabu hiyo ilimsaini Okwi mnamo July 2015 kwa mkataba wa miaka 5 akitokea klabu ya Simba SC ya Tanzania bara. 

Katika dirisha la usajili lililopita kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo alikuwa njiani kurejea Msimbazi, hata hivyo ilishindikana kutokana na ada ya usajili waliyokuwa wanataka Sonderjyske Fodbold. 

Baada ya miaka 11, Man Utd yarudi kileleni kwenye listi ya utajiri

$
0
0

Baada ya miaka 11, hatimaye Klabu ya Manchester United imerudi kileleni mwa listi ya vilabu tajiri duniani. United imepata mapato makubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita kulingana na taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani (Deloitte).


Manchester United imewashinda Real Madrid waliofanya vizuri katika michezo kwa miaka 11 baaada ya kukusanya mapato makubwa ya takribani Euro 689 katika msimu wa 2015-2016.

Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.

Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano kwa kutengeneza Euro milioni524 kwa msimu uliopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man City kuingia katika 5 bora.

Listi kamili ya Delloite Money League ipo hivi.


Ngasa amezungumzia kuhusu kutokea benchi Mbeya City

$
0
0
ngasa-2
Na Zainabu Rajabu
BAADA ya kutoka sare dhidi ya Azam, mshambuliaji wa Mbeya City FC Mrisho Khalfan Ngasa amesema mchezo ulikuwa mgumu kutoka na wapinzani wao kucheza kwa umakini licha ya kukosa nafasi nyingi za kufunga.
Ngassa ambaye alivunja mkataba wake na klabu ya  Free State  Stars Football Club  ya Afrika kusini kwa madai kwamba hawezi cheza timu ambayo haichukui ubingwa alitimkia kwenye falme za Kiarabu na kujiunga na Fanja FC ambako pia hakudumu kabla ya kutua Mbeya City.
Akizungumza baada ya mchezo wa Azam vs Mbeya Cuty kumalizika Ngasa alisema, mchezo ulikuwa wa kukamiana sana huku wakitengeneza nafasi nyingi lakini uimara wa beki ya Azam iliyokuwa  ikiongozwa na Agrey Morris ilikuwa makini kuokoa mipira yote ya hatari katika lango lao.
“Malengo tuliyojiwekea ni kumaliza mzunguko huu katika nafasi ya tatu na kuhakikisha mechi  zetu zilizobakia tunashinda na hilo tumedhamiria kujituma na kupambanana kadri ya uwezo wetu,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa  timu ya Yanga.
Ngasa ambaye amezichezea Simba, Yanga na Azam alisema, hashangai yeye kutokea sub ila ana amini ipo siku kocha wake atampa nafasi kwenye kikosi cha kwanza: “Ipo siku kocha wangu Kinnah Phiri ataona uwezo wangu na kunianzisha katika kikosi cha kwanza.”
 Mbeya City  ina point  25 huku ikiwa nafasi ya 7  katika msimamo wa ligi kuu na tarehe 28 itashuka dimbani  kumenyana na Prison.

Kampuni mpya ya betting imezinduliwa Dar

$
0
0

20170121_133350

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya Princess Bet imezindua duka jipya lililopo Sinza Afrikasana kwa ajili ya kutoa huduma za kisasa zaidi za kubeti ukilinganisha na wabetishaji wengine.

Meneja utawala wa kampuni hiyo Faraji Iddi amewaeleza waandishi wa Habari kuwa wamejipanga kutoa huduma za uhakika huku wale watakaoshinda mikeka hiyo wakipata pesa zao bila longolongo yoyote.

20170121_133740

“Huduma zetu ni bora, mteja ataweza kubeti sehemu yoyote huku akipata pesa yake muda huo huo tofauti na sehemu nyingine,” alisema Faraji.

Kwa upande wake Balozi wa PrincessBet Tanzania, Shaffih Dauda alisema kuwa mteja anaweza kubeti wakati mchezo unaendelea ambapo pia michuano ya ‘Sports Extra Ndondo Cup’ mashabiki wataruhusiwa kubeti.

Shaffih alisema wamejipanga kufanya mageuzi kwenye michezo hiyo ya kubeti na mteja anawezwa kulipwa kwa Tigo Pesa, M pesa au Airtel Money kuanzia wiki ijayo.

20170121_130513

Kampuni hiyo imewatoa hofu wateja wao kuwa hakuna atakayeshinda na kutopewa pesa yake kwakuwa wamejipanga na kwa siku kuna zaidi ya Sh. 25 milioni kwa ajili ya washindi.

Siri ya Oscar Joshua kucheza nafasi tofauti chini ya Lwandamina

$
0
0

oscar

Inawezekana na wewe ni miongoni mwa watu wanaojiuliza maswali kwa nini benchi la ufundi la Yanga limekuwa likimpanga Oscar Joshua katika nafasi tofauti na ile uliyozoea kumuona akiitumikia mara nyingi.

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema wanampanga Oscar Joshua kwenye nafasi tofauti kulingana na aina ya mchezo na wachezaji waliopo.

Kwenye mechi ya jana Jumamosi January 21, 2017, Oscar alipangwa katika beki ya kati sambamba na Dante wakati Yanga ikicheza mechi ya kombe la FA dhidi ya Ashanti United.

“Sio mara ya kwanza kwa Oscar Joshua kucheza katika namba tofauti. Kama unakumbuka, mechi yetu na TP Mazembe ugenini mchezaji wetu mmoja alipata kadi nyekundu Oscar akaingia kucheza kama beki wa kati.”

“Kutokana na mahitaji ya mechi na wachezaji waliopo Oscar leo alikuwa anafaa kucheza katika nafasi aliyocheza nadhani mmeona hajacheza kama mgeni katika hiyo nafasi.”

“Tunafurahi kuwa na mchezaji ambaye anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.”

Kama unakumbukumbu nzuri nadhani unakumbuka kwenye michuano ya Mapinduzi Cup ambapo Oscar alishapangwa kama mshambuliaji baada ya kutoka benchi kwenda kuchukua nafasi ya Juma Mahadhi.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Stars yupo hoi kitandani…

$
0
0

Tangu jana jioni kumekuwa na taarifa sambamba na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kueleza hali ya kiafya ya Godfrey Bonny mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.’

Godfrey Bonny amelazwa hospitali huko Rungwe-Tukuyu Mbeya ambako anapatiwa matibabu, jana Sports Extra ya Clouds FM ilizungumza na mdau wa soka ambaye aliwasiliana na dada yake Boni ambaye ndio anamuuguza kwenye hospitali ya Rungwe.

“Nimezungumza na dadayake Gedfrey Bonny anaitwa Neema Boniface amenifahamisha kwamba hali ya kaka yake (Godfrey) Bon si nzuri kabisa na kwa sasa hawezi hata kuzungumza. Nimemuuliza kuhusu taarifa za daktari amesema kwamba atapewa majibu ya X-ray siku ya kesho (leo) lakini hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza,” mdau aliyezungumza na dada yake Bon aliiambia Sports Extra.

“Kiujumla ni kwamba hali ya Godfrey Bonny sio nzuri kwa sababu nimezungumza na dada yake anaishia kulia na kunifanya nishindwe kupata majibu ya moja kwa moja.”

Kama una kiasi chochote au mchango wowote, unaweza kuwasiliana na dada yake Bonny au kutuma kwenye namba 0765 329 290 ya Neema Bonidace ambae ni dada yake Godfrey Bonny.

Mtandao huu umeona si busara kutumia picha za mgonjwa ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonesha akiwa amelazwa hospitali.

Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

shaffihdauda.co.tz inaungana na wadau wengine wa soka na michezo kwa ujumla kumtakia kila la heri Godfrey Bonny katika matibabu yake ili apone na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Timu yapigwa 8-0 ligi ya Zanzibar, Hilika kapiga hat-trick

$
0
0

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Baada ya mchezo uliopita kuvaa jezi sare na timu ya Mundu, na kuzikosa alama zote 3 pamoja na kupigwa faini ya shilingi 600,000 hatimae jana timu ya Kimbunga imejikuta inapata aibu nyingine baada ya kufungwa jumla ya mabao 8-0 kutoka kwa Zimamoto katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa saa 10 za jioni.

Katika mchezo huo nambari 170 ndio mchezo uliozaa magoli mengi kuliko yote ambapo Ibrahim Hamad Hilika akiondoka na mpira wake baada ya kupiga Hat-trick katika dakika ya 1, 27 na 64.

Mabao mengine ya Zimamoto yamefungwa na Hakim Khamis ‘Men’ dakika ya 40, 44, Khatib Said dakika ya 46, Idrissa Simai dakika ya 65 na Rashid Haji dakika ya 90.

Mechi nyingine zilizopigwa hapo jana mapema saa 8:00 za mchana Polisi na Chuoni walitoka sare ya 0-0, na mchezo wa usiku kati ya Jang’ombe Boys na Chwaka Stars wakamaliza kwa sare ya 1-1.

Chwaka ndio wa mwanzo kupata bao lililofungwa na Ali Hilali dakika ya 6 huku Hafidh Barik ‘Fii’ alisawazisha dakika ya 17 kwa upande wa Boys.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumamosi kati ya Kilimani City kukipiga na KMKM Saa 10:00 za jioni na mchezo mwingine Polisi dhidi ya Malindi saa 1:00 usiku.

Viewing all 565 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>