Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

PICHA 5: Shaffih Dauda alivyotua kwenye Rede Zanzibar

$
0
0

3-shafii

Na AbubakarKhatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Timu ya Muembe Laduimefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali katika Mashindano ya Nage (Rede) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 20-17 dhidi ya Kikwajuni Magic mchezo uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Tumbaku Miembeni Mjini Unguja.

5-shafi-na-muembe-ladu-1

Mchezo mwingine uliosukumwa mapema leo ni katiya Chuo cha Afya Mbweni dhidi ya Karakana City ya Chumbuni ambapo watoto wa Chumbuni wakawaonesha Nage safi wasomi wa Afya baada ya kushinda 12-9.

6-shafii-na-kikwajuni

Katika michezo ya leo Mgeni Rasmi alikuwa Shaffih Dauda ambae ni mwanamichezo nguli Tanzania, Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla ambapo pia ni Mkuu wa Vipindi vya Clouds Media Groups.

2-shaffi-anakaguwa

Dauda ameupongeza uongozi mzima wa Coconut Media Group kuandaa mashindano hayo ambayo yamekuwa gumzo Visiwani Zanzibar na nje ya Zanzibar kwa kusema kuwa atauchu masindano hayo na kueneza vizuri Tanzania bara.

1-shafii-dauda

Kesho saa 8 za mchana litaendelea pambano lililoshindwa kumalizika jana kati ya Miembeni na UVCCM Dimani ambapo mchezo mwingine utapigwa saa 10:15 za jioni kati ya Six Center na Kwalinato.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>