Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all 565 articles
Browse latest View live

Daktari kawatoa hofu wanasimba jeraha la Mkude “kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa”

$
0
0

Kiungo wa Simba Jonas Mkude ameumia kifundo cha mguu wa kulia (ankle) wakati wa mazoezi ya jioni ya klabu hiyo kwenye uwaja wa Boko Veterans, Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji.

Daktari wa Simba Yassin Gembe kupitia instagram account ya Simba amenukuliwa akisema amegundua majeraha ya Mkude sio makubwa sana na kutokana na anaendelea vizuri baada ya matibabu ya awali aliyompatia.

“Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa sana ila kesho tutatoa taarifa kamili kuhusiana na hali yake kwa ujumla.”

“Kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia.”

Afisa habari wa Simba Haji Manara pia ame-post taarifa iliyotoka kwa daktari Gembe kwamba Mkude huenda akawa nje ya uwanja kwa siku mbili hadi tatu.

“Kwa mujibu wa daktari wetu, injury ya Jonas ni ndigo. Anasema maximum anaweza kuwa nje kwa siku mbili hadi tatu, hii ndiyo taarifa rasmi ya klabu toka kwangu”-Haji Manara.


Samatta, Kichuya, waiua DR Congo ya mastaa

$
0
0

Magoli mawili yaliyofungwa na nahodha Mbwana Samatta na Shiza Kichuya yameipa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya DR Congo kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya fifa uliochezwa uwanja wa taifa.

Ushindi huo umekuja baada Stars kupoteza mchezo wake wa kirafiki ugenini kwa kufungwa 4-1 na Algeria Machi 22, 2018.

DR Congo ikiwa na wachezaji wake wengi wanaocheza Ulaya kama Yannick Bolasie (Everton), Afobe Benik (Wolves) Chancel Mbemba (Newcastle United) na wengine wengi lakini Stars ambayo inamchezaji mmoja anaecheza Ulaya (Samatta) imeweza kuibana DR Congo na kupata ushindi.

DR Congo ni timu bora Afrika, inashika nafasi ya tatu nyuma ya Tunisia na Senegal, ipo nafasi ya 39 katika viwango vya Fifa vya mwezi Machi 2018 hivyo Stars imepata matokeo dhidi ya timu bora Afrika na Duniani.

Hadi sasa  tanzania ipo nafasi ya 146 katika viwango vya Fifa vilivyotolewa mwezi machi 2018 ikiwa inapambana kusogea nafasi za juu kwa kucheza mechi zakirafiki za kimataifa dhidi ya timu ambazo zipo  katika nafasi za juu.

SIO ZA KUKOSA: mechi za kukata na shoka

$
0
0

Bila shaka makocha wengi kwa sasa watakuwa wanakenua. Wachezaji wachache sana tumepokea taarifa za majeruhi. Naam. Kipute cha ulaya kimerudi sasa. Ule mchezo wa kujaribisha mapanga kwenye migomba umekwisha. Wikiendi hii kutakuwepo na vipute vya kukata na shoka.

Baadhi tu hizi hapa.

March 31: Everton vs Man City


Mechi hii ni mechi muhimu sana kwa Man City na ni mechi muhimu sana kwa Mashabiki wa Man United. Kama City atashinda mchezo huu basi mchezo unaofuata wa Man United dhidi ya Man City itakuwa mechi ya kukabidhiwa ubingwa. ni fedheha kubwa ndani ya Manchester Derby, Man united kutoa nafasi ya bingwa ambae ni mpinzani wake mkubwa. Safari ya kwenda kutawazwa mabingwa kwenye Derby yao itafanikishwa na karamu ya ushindi watakayopata Goodison Park.
March 31: Sevilla vs Barcelona


Barcelona wana tatizo la majeruhi kwa sasa. Wasiwasi mkubwa ni suala la Messi kama atakuwa fiti au lah. Sergio Busquets bado atakuwa nje ya uwanja kwa matatizo ya mguu. Blaugrana watasafiri kwenda mpaka kunako Estadio Ramón Sánchez Pizjuán. Sevilla wametoka kupata ushindi mnono kabisa dhidi ya Man United katika uga wa Old Trafford hivyo watakuwa na hamasa kubwa sana.

March 31: Juventus vs Milan

AC Milan wametoka kuadhibiwa na Arsenal nje ndani lakini vijana hawa wa Rossoneri watahitaji kupigania nafasi ya 4 kupata nafasi ya kushiriki tena michuano ya UEFA mwakani. Sala za Kocha mkuu wa Napoli Maurizzio Sarri zitakuwa upande wa Gattuso atakapohitaji Ac Milan kushinda au Kutoka Sare. Juventus wameipita Napoli Alama mbili tu hivyo watahitaji kwenda juzi zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa.

March 31: Bayern Munich vs Dortmund 

Ni mchezo wa mahasimu wa muda mrefu. Mchezo huu hautoi uelekeo wa ubingwa ila watacheza kwa ajili ya heshima za pande zote mbili. Dotmund atapigania nafasi ya pili ili kumpa Schakle nafasi ngumu ya kumfikia.

March 31: LA Galaxy vs Los Angeles FC

Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Zlatan Ibrahimovic akiwa na La Galaxy. Mashabiki wanaomkubali Zlatan watatazamia Derby hii kubwa Marekani. Sio mchezo wa kuvutia sana duniani lakini ujio wa Zlatan utabadilisha upepo wa watu wa Sweden

March: Arsenal vs Stoke City

Wazee wa unga unga mwana. Mchezo mwingine wa kukata na shoka. Arsenal hawajui kesho kuhusu UEFA. wapo wapo tu. Mchezo muhimu kabisa kwenye kumalizia ligi. Piga ua lazima Arsenal washinde mchezo huu. Stoke ni moja ya timu ngumu. Tuone itakuwaje
Sunday, April 1: Chelsea vs Tottenham

Kama kuna mechi itamtoa Conte kijasho chembamba basi ndio hii. Manara angekuwa msemaji wa FA basi angesema This is London derby. Hii ni ile mechi ya unatoa au hutoi. Tottenham wapo juu kwa tofauti ya alama 5 dhidi ya Chelsea. Kama Chelsea atapoteza mchezo huu nina uhakika wasilimia 90 kuwa hawatashiriki UEFA mwakani. Kama Tott atashinda basi atakuwa ameweka gepu la alama 8.

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Uchunguzi unaendelea uraia wa kigogo TFF

$
0
0

Idara ya uhamiaji nchini bado inaendelea kuchunguza uraia wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao, afisa habari wa uhamiaji Ally Mtanda amesema uchunguzi bado unaendelea na utakapo kamilika watatoa taarifa rasmi.

“Bado tunaendelea na suala lake la uchunguzi na litakapokuwa tayari tutawaarifu, masuala ya uchunguzi hatuwezi kuyaweka wazi hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha ndipo mambo yote yatakuwa hadharani.”

“Wanamicheo wawe na uvumilivu muda sio mrefu mambo yote tutayaweka wazi.”

Mara kadhaa Kidao amekuwa akihojiwa na idara hiyo kutokana na kinachoelezwa kuwa ni kuchunguzwa uraia wake.

Wambura aitwa kujua mbivu na mbichi

$
0
0

Kamati ya rufaa ya maadili ya shirikiso la soka Tanzania TFF imetangaza kukutana Jumamosi kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura aliyefungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya soka.

Kaimu afisa habari wa TFF Clifford ndimbo amethibitisha kuhusiana na taarifa hiyo.

“Kamati ya rufdaa ya maadili inataraji kukaa Jumamosi ya Machi 31 ambapo itakuwa saa 5 asubuhi, pamoja na mambo mengine pia itasikiliza rufaa ya Michael Wambura ambaye alikata rufaa.”

“Anaruhusiwa kuja kutoa utetezi wake kwa njia ya mdomo, maandishi au kuleta vielelezo vyote vya utetezi wake pia anaweza kuleta mwakilishi akiwa na barua ya uwakilishi au anaweza kuamua kutokuja kabisa.”

“Tayari wito wake ameshapelekewa na bila shaka atakuwa amesha upokea, kuelekea katika shauri hilo siku ya Jumamosi gharama zitakuwa juu yake mwenyewe.”

Wakili wa Wambura Emanuel Muga amesema mteja wake amepokea wito kutoka kamati ya rufaa ya maadili na atakwenda kutetea haki yake mbele ya kamati hiyo.

“Ni kweli Michael Wambura amenieleza kwamba amepata wito na wito huo ni kwa ajili ya kikao cha Machi 31 saa 5 asubuhi pale TFF atakapoenda kusikilizwa.”

“Wambura amesema yupo tayari kwenda kutetea haki yake mbele ya kamati na ana hoja zake na amethibitisha kwamba atakwenda.”

Azam yabaki njia moja kimataifa

$
0
0

Mtibwa Sugar imeiondosha Azam kwenye michuano ya kombe la shirikisho Tanzania bara ‘Azam Sports Federation Cup’ kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani ya dakika 90.

Azam ambayo ilishiriki michuano ya kimataifa msimu uliopita inabidi ishinde taji la ligi kuu Tanzania bara ili kuweza kucheza mashindano ya Afrika msimu ujao.

Ipo nafasi ya nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 22 nyuma ya Yanga na Simba ambazo zina pointi 46 huku Yanga ikiwa imecheza mechi 21 wakati Simba yenyewe imecheza michezo 20.

Mibwa Sugar inaungana na Stand United na JKT Tanzania ambazo zimeshafuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo bingwa anaiwakilisha Tanzania bara kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika.

Jumapili Aprili 1, 2018 utachezwa mchezo mwingine wa robo fainali ya ASFC kati ya Singida United na Yanga ambapo mshindi atakamilisha idadi ya timu nne zitakazocheza hatua ya nusu fainali.

Mambo matatu anayofanya Juma Mahadh kabla ya mechi

$
0
0

Kila mtu ana utaratibu wake aliojiwekea kwenye maisha ya kila siku, kwa upande wa kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadh yeye ana utaratibu wake pia kabla ya kwenda uwanjani kutekeleza majukumu yake ya kazi.

Kabla ya kila mechi Mahadh hufanya mambo matatu ambayo ni muhimu kwake na anaamini yanamchango mkubwa kwake na kwa timu yake.

Mahadh amezungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ na kutaja vitu vitatu ambavyo huvifanya kabla ya mechi.

“Kabla sijaondoka hotelini lazima niombe Mungu kwanza, halafu namjulisha mama yangu kwamba naenda kwenye mechi aniombe baada ya hapo ni visingeli mwanzo mwisho.”

Unaweza ukajiuliza ni kwa nini anasikiliza muziki wa singeli na si aina nyingine ya muziki, mwenyewe amesema kwa sababu muziki huo huwa unaamsha mzuka.

“Singeli ni muziki wa kuamsha-amsha, sisi tunaenda kwenye mechi ambayo ni mchezo wa kuchangamka kwa hiyo inabidi upate kitu kitakacho kuchangamsha.”

Mwanzoni mwa mwaka huu aliandika waraka wa kuomba radhi kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga kuhusu kila kitu ambacho kilitokea nyuma na kuamua kuanza upya. Mkazuzu amemuuliza maendeleo yakoje tangu aamue kuanza upya.

“Namshukuru Mungu kila kitu kinaenda vizuri na nashukuru watu nilionao sasa hivi wananipa sapoti na hamasa kunifanya niwe najitihada zaidi kwa sababu naamini mwanzo nilikosea lakini nimeamua kujirekebisha na watu nilionao ninsahihi.”

Wambura ndio basi tena

$
0
0

Kamati ya rufaa ya maadili ya TFF imetupilia mbali rufaa ya Michael Wambura aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF ambaye alifungiwa maisha kujihusisha na shughuli za soka.

Baada ya kupitia hoja zake za rufaa, kamati ya rufaa ya maadili imejiridhisha na maamuzi ya awali yaliyotolewa na kamati ya maadili kumfungia maisha Michael Wambura.

Kamati ya rufaa yamaadili imeiagiza TFF kulifikisha suala la Wambura kwenye vyombo vya sheria.


Sababu iliyomfanya Kamusoko ajifunze Kiswahili

$
0
0

Jambo ambalo hutakiwi kufanya ni ‘kumteta’ Thabani Kamusoko kwa lugha ya Kiswahili ukiamini ni raia wa kigeni na hatoelewa unachozungumza, utakuwa umefeli jamaa ni anatwanga kiswahili hadi cha mtaani.

Kiungo huyo wa Yanga toka Zimbabwe anapozungumza Kiswahili huwezi kujua kama si raia wa Tanzania, Kamusoko yupo vizuri kwa Kiswahili asikwambie mtu.

Wakati anafanya mahojiano na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ mjini Morogoro ambako Yanga iliweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Wolaitta Dicha, alisema hakuna mwalimu aliyekuwa akimfundisha bali aliamua tu mwenyewe kujifunza Kiswahili.

Katika mazungumzo hayo, Kamusoko akafunguka sababu kubwa iliyomfanyabaamue kujifunza Kiswahili, kumbe ni ishu ya kumrahisishia mawasiliano awapo kazini akisukuma gozi.

“Mpira unahitaji mawasiliano kwa kiasi kikubwa, pia unahitaji kuzungumza lugha moja kwa hiyo niliamua kujifunza Kiswahili ili tuelewane vizuri”-Thabani Scara Kamusoko kiungo Yanga SC.

Hivi karibuni Method Mwanjale ni mchezaji mwingine ambaye anatoka Zimbabwe aliyekuwa anazungumza Kiswahili kwa ufasaha ukiachana na akina Niyonzima, Tambwe, Mavugo ambao nchi zao zinazungumza pia Kiswahili.

kwani Yanga na Welayta kuliendaje?

$
0
0

Mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Yanga na Wolayta Dicha SC kutoka Ethiopia umekamilika. Yanga waliweza kupata ushindi wa magoli mawili kwa bila na kujiweka mguu mmoja mbela katika hatua ya makundi. wahabeshi walishindwa kabisa kuipenya ngome ya Dante na Ninja. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yalijitokeza katika mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Yanga na Welayta Dicha.

Walinda lango?

Youthe Rostand aliweza kuchomoa michomo minne licha ya kufanya uzembe mara moja. Golikipa wa Wolayta Wondwosen Geremew aliokoa mipira mitatu na hakufanya uzembe wa aina yoyote.

Safu za ulinzi zilikuwaje?

Timu zote zilikuwa imara katika kuzuia mashuti. Yanga waliweza kuzuia (kublock) mashuti 6, Welayita walizuia mara 6. Andrew Vicent Dante na Abdal shaibu Ninja walifanya kazi ya ziada kwa kuhakikisha mkameruni hatari Arafat Djako na Yared Dawit Yarfo kuonekana kama watazamaji tu. Yanga waliweza kuondosha mashambulizi yaliyonekana kuwa namadhara makubwa katika eneo la hatari mara 10 huku waethiopia wakiondosha mara 4.

PATA KIFURUSHI

Jina la Utani Bees of Tona

Uwanja wao Wolayta Sodo

Kocha; Zenebe Fisseha

Umiliki wa mpira na Eneo la kiungo

Bila shaka Wwaethiopia walitawala sana eneo la kiungo kwani walikuwa na uwezo mzuri wa kumiliki mpira. mchezo wao mwisho dhidi ya Zamalek kocha wao aliwaambia waandishi ha habari kuwa hawataenda kuzuia ugenini mara baaa ya kupata ushindi nyumbani. Kocha huyu mpya wa Wolayta dicha anaoenakana kuwa anajiamini sana.

Katika mchezo huu Yanga walitumia zaidi mipira mirefu ili kuwatafuta washambuliaji wao. Yanga walicheza mipira mirefu ya malengo mara 24 huku Welayta Dicha wao kipindi cha kwanza hawakucheza mipira mirefu sana lakini kipindi cha pili baada ya kuona hali mbaya walibadilisha mfumo wao na kuacha mipira mirefu mara 9.

Mara ya mwisho Yanga kufuzu hatua ya makundi ilikuwa mwaka 2016 ilipopangwa na Medeama (Ghana), TP Mazembe (DRC Congo), na Mo Bejaia (Algeria).

Safu ya ushambuliaji.

Ibrahim Ajibu pamoja na Yusuph Mhilu walijitahidi sana kutengeneza nafasi nyingi za magoli. Yanga walitengeneza nafasi muhimu takribani 13 huku wapinzani wao wakitengeneza nafasi 4. Yanga walipiga mashuti takribani mashuti 14 na mashuti 4 yalilenga golini, Welayta wakapiga mashuti 8 na 5 yalielekezwa kwenye lango la Yanga. Yanga walifanikiwa kupata kona 7 sawa na welayta. Yanga walifika langoni mwa Welayta nara 73 huku Welayta wao wakijaribu mara 65.

Nidhamu ya mchezo.

Mpira ulikuwa mzuri na kuvutia. Hakukuwa na zile rabsha za vurugu kutokana na mfumowa wapinzani wa Yanga. a. Aina hii ya mchezo ulifanya mchezo kutulia kwani Yanga waligundua tatizo la Welayta. Yanga walicheza rafu mara 9 na Welayta nao walipata. Hakukuwa na kadi na ni mchezaji mmoja tu aliyetolewa nje kwa majeraha.

Ilikuwaje Yanga wakafanikiwa? Wapinzani wa Yanga walikuwa na miili midogo sana. Walicheza mchezo wa pasi nyingi ili kukwepa mpira wa nguvu kwani hawakuwa na miili ya kucheza aina hiyo ya mpira. Kimo cha wachezaji hawa wa Welayta ndio alikuwa mchawi wao. Yanga walifanikiwa kupiga krosi 15 na krosi mbili zilazaa matunda. Welayta sio warefu ni wafupi na Yanga waligunuda hilo mapema. Yanga wanapaswa kutumia mfumo huo wa mipira ya juu kule sodo stadium

Uzuri wa Welayta?

Walianza kwa mbwembwe sana, wakawa makini kwenye upigaji wao wa pasi. Walikuwa na wastani wa pasi 10 kwenye nusu ya uwanja wa Yanga, huku yanga wakiwa na wastani wa pasi tano pekee kwenye nusu ya upande wa Welayta hasa kwa kipindi cha kwanza. Walikuwa wanabembeleza sana. Na walichelewa kubadilika kwani walicheza kwa kujiamini kiasi cha kupitiliza.

Ushauri?

Yanga wawe makini sana katika mchezo wa marudiano. Takwimu zao zinaonesha kuwa michezo yao minne ya mwisho hawajapoteza nyumbani.

Takwimu zote na makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram) (0763370020)

IMETHIBITISHWA: Lwandamina ameitosa Yanga

$
0
0

Imethibitika kwamba aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amerejea kwao Zambia na amejiunga rasmi la klabu yake ya zamani ZESCO United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kujiunga na Yanga.

Mwandishi wa habari za michezo nchini Zambia anayefahamika kwa jina la Sam amethibitisha kwamba klabu ya ZESCO imemtangaza rasmi Lwandamina kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo.

“Lwandamina ametangazwa rasmi kwamba amerejea ZESCO United leo. Baadhi ya mashabiki hawajafurahia kwa sababu wanamkubali sana kocha aliyeondoka (Tenant Chembo) ambaye alikuwa msaidizi wa Lwandamina. Baada ya Lwandamina kuondoka, Tenant Chembo aliendelea kubaki kama kocha wa muda kwa kipindi chote hicho.”

“Chembo ameamua kujiuzulu kwa sababu ZESCO iliendelea kumfanya kocha wa muda lakini baadaye alipata timu nyingine na kuamua kuachana na ZESCO.”

Novemba 25, 2016 Lwandamina alitambulishwa mbele ya waandishi wa habari kama kocha mkuu wa Yanga akichukua nafasi ya Hans van Pluijm. Ilielezwa Lwandamina alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Habibu Kyombo asiyependa bata alivyoamua kuichagua Singida na kuitosa Simba

$
0
0

Zoezi la usajili linazidi kupamba moto huku vilabu vya Simba, Singida United na Azam vikionekana kufanya usajili mapema tofauti na timu nyingine.

Mshambuliaji aliyesajiliwa na Singida United hivi karibuni Habib Kyombo amevunja ukimya nakuzungumza baada ya usajili wake.

“Kwangu naamini Singida itakuwa klabu na wachezaji nitakaokutana nao tutafanyakitu kizuri kuweza kuisaidia timu kupata matokeo na mataji.”

Kuna tetesi zilimhusiah Kyombo kutakiwa na Simba na Azam lakini mwisho wa siku akasaini Singida, mwenyewe anasema muda bado wa kwenda Simba, Yanga na Azam.

“Ukisema timu kubwa hata Singida nayo piani timu kubwa, halafu ni timu ambayo naweza kupata muda mwingi wa kucheza. Haimaanishi ningeenda sehemu nyingine nindeshindwa kucheza ila Simba na Yanga timu kubwa na kila mtu anatamani kwangu mimi naona muda bado, ukifika nitacheza.”

Kyombo ameingia fainali (wachezaji watatu wa mwisho) kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa VPL, hatua hii imemuongezea chochote?

“Imeniongezea vitu vingi, kwanza kujituma zaidi kwa sababu kuwa miongoni mwa hao si kazi ndogo unatakiwa kujituma ili msimu ujao nipate zaidi ya hiki.”

Anapambana na Shabani Idd Chilunda (Azam) Yahya Zayd (Azam) lakini Kyombo anaamini yeye ni bora na anastahili kushinda tuzo hiyo.

“Ni wachezaji wazuri, wana kila sifa kakini mimi pia ni mchezaji mzuri nadhani nastahili kushinda hiyo tuzo kwa sababu nimefanya vizuri.”

Hafagilii ‘bata’ bata kabisa

“Nashinda home naangalia movies, nacheza game, jioni naenda mazoezi kidogo siku yangu inakuwa imeisha hivyo huwa sitoki.”

“Kupumzika pia ni bata kwa hiyo inategemea tu mwenyewe, naamini ukipumzika ni zaidi ya bata kwa hiyo kwangu kupumzika ni bora zaidi.”

Kama hujui, Kyombo kabla ya kujiunga na Mbao amepita kwenyentimu nyingi. Alianzia BQ Academy ampo alilelewa kwa miaka nane halafu akajiunga na Simba B ambapo hakukaa sana akasajiliwa na Lipuli akacheza mzunguko wa kwanza mzunguko wa pili akaenda zake Mbao.

Maelfu wahudhuria mashindano ya mbio za Mbuzi Dar

$
0
0

Fursa ya kwanza ya uandaaji wa mashindano maarufu ya mbio za mbuzi imekuwa ya mafanikio kwa Klabu ya Rotary ya Oysterbay. Tukio hilo lenye burudani ya aina yake lilikwenda kwa Motto wa ‘Wakanda Goat are You’, na kuvuatia watu zaidi ya 4,500 waliokusanyika katika eneo la The Green, Oysterbay kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo.

Matukio muhimu yaliyofuata baada ya mbio hizo ni mchezo wa bahati nasibu ambao uliwezeshwa na wafadhili wa hapa nyumbani pamoja na gwaride la kuonyesha mavazi, ambapo watu mbalimbali walipata fursa ya kuonyesha mavazi yao aina ya Wakanda kwa kurejelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.

Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwa wamewabeba mbuzi wao tayari kushiriki mbio hizo wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Ni mwaka wa kumi na nane mfululizo wa mashindano hayo lakini kwa mwaka wa kwanza chini ya Rotary Goat Races, tukio hili maarufu la kifamilia lilivutia maelfu ya watu siku ya tarehe 23 Juni. Tukio hilo likifanyika katika eneo la ‘The Green’ chini ya motto wa ‘Wakanda Goat are You”, wahudhuriaji walifurahia aina saba za mbio, vyakula vya aina mbalimbali vya hapa nyumbani, zawadi kubwa mbalimbali za bahati nasibu, michezo ya kuweka dau na gwaride la ushindani la mavazi ya Wakanda.

Mashindano hayo yalianza kwa mbuzi kusimama kwenye mstari wa mwanzo wa mashindano, huku watazamaji wakivuta pumzi kuona mbuzi wanavyopigania ushindi wa kuwa namba moja.

Katika raundi ya kwanza Mbuzi aliyeibuka kidedea ni namba 8 ambapo zawadi yake ilidhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya CocaCola, Raundi ya pili mbuzi namba 7 aliibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na East Africa TV/Radio huku raundi ya tatu mbuzi namba tisa akikiibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na Kampuni ya Aggreko.

Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwakimbiza mbuzi wao wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Wamiliki wa mbuzi hao walisherehekea ushindi huo kwa staili ya kipekee na watu ambao waliweka dau kwa mbuzi hao kushinda walipokea fedha zao za dau hilo. Katikati ya mbio hizo, michezo ya bahati nasibu kwa washindi wa zawadi kubwa pia ilifanyika na washiriki kadhaa kushinda. Watoto pamoja na watu wazima walipendezesha gwaride la mavazi na kujishindia zawadi kabambe kwa mavazi hayo. Ni wazi watoto walifanya vizuri zaidi kwenye kipengele hiki.

Viongozi wa mashindano ya mbio za mbuzi, Abdulrahman Hussein na Mathew Hellela walifurahishwa na mwitikio mkubwa wa watu.

“Ni mara yetu ya kwanza kuandaa mashindano haya ya mbio za mbuzi na tunafuraha kuwa tukio hili limekuwa la kufana sana kwa kila mhudhuriaji na pia kwa watu kutuamini katika kuwapa kitu kikubwa na cha tofauti kwa mwaka huu”, alisema Abdulrahman Hussein.

Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwakimbiza mbuzi wao wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

“Pia inaonyesha kuwa timu yetu ya kujitolea, ambayo ilitumia mwezi mzima kuandaa tukio hili, ilikuwa kwenye njia sahihi na nguvu zao leo zimelipa kwa kuwapa wakati mzuri  wahudhuriaji wote”, aliongeza Hussein.

Kwa upande wake Mathew Hellela aliwashukuru wafadhili wote kwa imani na misaada yao.

“Tulikuwa wapya katika kuandaa tukio la namna hii na tunashukuru sana kwa imani ambayo wafadhili wametupatia sisi watu wa Klabu ya Rotary katika kufanya jambo lililo sahihi. Mwaka huu ulikuwa mwanzo mzuri na tunatarajia kubeba mafanikio haya kwa miaka ijayo ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary.”

Baadhi ya watoto na watu wazima wakionyesha mavazi yao aina ya Wakanda wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary, Oysterbay alisema kuwa anajivunia sana timu yake na anasubiria kwa hamu kutekeleza miradi ya elimu ambayo Klabu yake itaifanyia kazi hivi karibuni, kwa kutumia mapato ya mbio hizo. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.

Mashindano ya mbio za mbuzi kwa mwaka huu yamefadhiliwa na Resolution Insurance, SWISS, Toyota, Coca Cola, East Africa TV/Radio, Aggreko, SBL, Mastercard, Le Grand Casino na Red ‘n White. Michango ya ukarimu pia imetoka kwa JC Decaux, PM Group, Almar Containers TZ, SBS, Abstrat, The Slipway Hotel na  Pizza Hut pamoja na Advertising Dar, ALAF-Safal Group, Britam Insurance, Selcom Paytech, VClick Professional Photography, WS Insight, Green Waste Pro na CAPS Limited.

Baadhi ya watoto na watu wazima wakionyesha mavazi yao aina ya Wakanda wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Michezo ya bahati nasibu ilipewa nguvu na SWISS, SBL, The Sea Cliff Hotel, The Slipway Hote, Zen Spa, Engen, Coastal Airlines na 305 Karafuu Restaurant. Michango mingine ilitoka Kwa kampuni za:-Jumia, Advertising Dar, Splendid Cleaners, TAN Management – Insurance broker, Merrywater, Vet Care, Dar Signs, Karafuu Restaurant, Prime Advertising, Reader Rabbits, World Link.

Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za wilaya za kupanda miti.

Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii.Mapato yote ya mbio za Mbuzi za Rotary yatatumika kwenye miradi ya elimu ya Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kama mpango wa ufadhili wa elimu ambao unawasaidia wanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Tanzania, nipe fagio na Shule ya Msingi Msasani.

Baadhi ya watoto na watu wazima wakionyesha mavazi yao aina ya Wakanda wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’?

Rock City Marathon yazinduliwa Mwanza

$
0
0

Msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa rasmi jijini Mwanza mwishoni mwa wiki hii huku wito ukitolewa kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.

Uzinduzi  wa mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA)  ulihusisha pia wawakilishi wa wakuu wa mikoa yote ya kanda ya Ziwa ikiwa ni mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kagera.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw Mongella katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini humo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha alisema ipo haja ya wadau wa utalii na michezo katika kanda hiyo kuhakikisha kwamba  wanayatumia vizuri mashindano hayo katika kuhakikisha fursa na vivutio vya utalii vilivyopo kwenye ukanda huo vinatangazwa ipasavyo.

“Ndio maana serikali tunafarijika sana tunapoona sekta binafsi inajiinua na kubuni mbinu bora kabisa hasa kupitia michezo ili kuiboresha zaidi sekta hii ya utalii hususani kwa kanda yetu ya Ziwa ambayo kwa sasa ipo kwenye  mabadiliko makubwa,’’ Alisema.

Akizungumzia maendeleo ya mchezo huo Bi Tesha alisema   ipo haja kwa wadau kuhakikisha wanatumia vizuri mwamko wa mkubwa mashirika na taasisi mbalimbali hapa nchini ambazo zimeamua kuunga mkono mchezo huo katika kuinua vipaji vipya.

Niombe sana kila kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia mchezo huu katika ngazi tofauti tofauti, idara mbali mbali na vyama mbali mbali, tulirudishe  taifa kama  ilivyokuwa  miaka  ya  nyuma.’’ Alisema.

Mbio hizo zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA Energy Tanzania, New Mwanza Hotel, Precision Air, KK Security, CF Hospital, Rock City Mall, Dasani, Metro Fm, Global Education Link, Barmedas TV, Gold Crest Hotel, NSSF, EF Outdoor, na SDS huku wengine wakionyesha nia ya kudhamini mbio hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi  alisema uzinduzi wa mbio hizo zinazotarajia kufanyika  Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umefanyika mapema ili kuruhusu wadau wote wapate muda wa kutosha katika kujiandaa kwa ajili ya ushiriki.

“Lakini pia katika msimu huu wa mbio hizi tumefungua milango zaidi kwa wadau wa maliasili na utalii ambapo si tu kwamba wataweza kushiriki katika mbio hizo bali pia watapata fursa ya kufanya maonyesho ya utalii  pamoja kutoa elimu zaidi kuhusu fursa za kitalii pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.’’ Alisema.

Alisema kanda ya Ziwa kwa ujumla  ina vivutio vingi  vya kihistoria ambavyo vinaweza kutumika kuimarisha sekta ya utalii wa ndani na nje huku akiongeza kuwa ukaribu uliopo baina ya jiji la Mwanza na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni sababu tosha ya mji huo kuvutia watalii wengi zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine iliyo nje ya kanda ya Ziwa.

Ofisi ya Marathon Mwanza yazinduliwa

$
0
0

Hatimaye ofisi za Rock City Marathon zimezinduliwa rasmi jijini Mwanza ambayo itakuwa ikihudumia mikoa yote iliyopo Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha amezindua ofisi hizo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Uzinduzi wa mbio hizo zinazotarajia kufanyika  Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umefanyika mapema ili kuruhusu wadau wote wapate muda wa kutosha katika kujiandaa kwa ajili ya ushiriki.


Kim kajiuzulu TFF

$
0
0

Mshauri wa ufundi wa TFF kwa timu za vijana Kim Poulsen amejiuzulu nafasi yake.

Kim amezungumza na The Citizen na kusema amejisikia vibaya kuchukua  uamuzi huo ambapo anawaacha vijana wenye vipaji wa U-16, Serengeti Boys ambao walishinda ubingwa wa CECAFA kwa vijana wa U-17 mwezi Aprili mwaka huu.

Kim amesema alikuwa anafurahia maendeleo ya vijana licha ya changamoto alizokuwa akikutana nazo ndani ya TFF.

“Nasikitika kutangaza hivyo kwa sababu nawaacha vijana waliozoea kuwa pamoja kwenye kila hali. Wakati mwingine unalazimika kufanya maamuzi ambayo kila mtu atauliza kwa nini umeamua kufanya hivyo. Nawatakia kila la heri wachezaji wangu na wadau wa soka”-Kim.

Kim hakuwa tayari kutaja sababu iliyopelekea kujiuzulu: “Nilichohitaji kukueleza ni kuhusu kujiuzulu kwangu, kama itahitajika kueleza kwa nini labda itakuwa baadaye lakini kwa sasa ni maamuzi yangu kuhusu kazi yangu.”

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao hakuwa tayari kuzungumzia juu ya kujiuzulu kwa Kim. “Tuna ofisa habari wetu ambaye anaweza kufafanua jambo hilo, wasiliana naye tafadhali”-Kidao.

Ofisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema hana taarifa kuhusu kujiuzulu kwa Kim.

Mwaka 2011 Kim aliajiriwa kama kocha wa timu ya taifa ya vijana kabla ya kupewa majukumu ya kuifundisha Taifa Stars 2012 akichukua nafasi ya m-denmark mwenzake Jan Poulsen.

Mwaka 2014 mkataba wake ulivunjwa na uongozi mpya wa TFF ulioingia madarakani chini ya Rais wa wakati huo Jamal Malinzi. Miaka miwili baadaye (2016) Kim aliitwa kwa mara nyingine kuendelea na majukumu ya kuwa mshauri wa ufundi wa timu za vijana.

Mwaka 2017 akiwa na Bakari Shime, Kim aliisaidia Serengeti Boys kufuzu kushiriki fainali za AFCON kwa vijana wa U-17 nchini Gabon.

Source: www.thecitizen.co.tz

Ndoto ya Kiemba kwa Himid imetimia

$
0
0

October 2016 katika mishemishe zangu kwenye mitaa ya Shinyanga mjini nilikutana na Amri Kiemba miongoni mwa viungo bora kuwahi kuwashuhudia Bongo.

Kiemba alikuwa gym anajiweka fit kwa sababu wakati huo alikuwa anaitumikia Stan United ‘Chama la Wana’.

Katika story zetu za hapa na pale nikamuomba anitajie wachezaji watatu wanaomvutia kwenye soka la ndani.

Alichonijibu Kiemba ni kwamba, ana heshimu uwezo wa kila mchezaji kwa sababu kila mtu ana ‘strength na weaknesses’ lakini akasema anavutiwa na Himid Mao ‘Ninja’ kwa sababu anacheza mpira wa ushindani sana ambao hauwavutii mashabiki lakini unaleta matokeo.

“Mimi kama mchezaji namuelewa sana Himid Mao kwa sababu anacheza mpira wa kutafuta matokeo sio wa kuwapendeza mashabiki.”

Kiemba akaniambia katika vijana ambao anapenda awaone wanacheza nje ya nchi ni pamoja na Himid Mao kwa sababu ana moyo wa kushindana.

“Kwa hiyo katika vijana, ningependa Himid atoke Tanzania kwa sababu ana moyo wa kushindana kuliko kufurahisha mashabiki ambao ndio mpira wetu sisi.”

Kwa sasa huenda Kiemba anafuraha na amani kwa sababu alitamani kuona Himid anacheza nje ya Tanzania na jambo hilo limefanikiwa, hivi karibuni ‘Ninja’ alisaini mkataba wa miaka mitatu na Petrojet ya Misri.

Aliwataja pia Haruna Moshi Boban na Athumani Idd Chuji kama wachezaji bora wa kizazi chao.
#Ligend

Abdi Banda! Hakamatiki tena! anatafutwa na mabingwa

$
0
0

Kupitia jarida maarufu la habari ncini Afrika Kusini Soccerladuma limeripoti kuwa mlinzi mahiri wa klabu ya Baroka Fc Abdi Banda a.k.a Abdi “Van Djik” anawindwa na mabingwa wa msimu na mabingwa mara 8 wa ligi kuu Afrika kusini Mamelodi Sundowns.

Mabingwa Mamelodi Sundowns wapo katika harakati za kuimarisha kikosi chao baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.

Taarifa kutoka Siya , Masandawana zinadai kuwa Abdi Banda anahitajika na klabu hiyo baada ya kufanya vyema na klabu yake licha ya matokeo ya kusuasua ya klabu hiyo ya msimu uliopita waliomaliza nafasi ya 2 kutoka mkiani wakiwa wameruhusu mabao 38.

Baroka FC watotto hawa wanaotumia uwanja wa Old Peter Mokaba huu ni msimu wao watatu kwenye ligi hiyo.

Hata hivyo huenda dili hili likawekwa kwenye wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kuhitaji huduma za mlinzi huyo.

Morgan Mammila ambaye ni mkurugenzi wa klabu hiyo alisema kuwa klabu uake haitaruhussu mchezaji yeyote kuondoka na watapambana kumaliza nafasi nane za juu msimu ujao.

“Malengo yetu ni kucheza vyema na kuhakikisha hatutaruhusu mchezaji yeyote kuondoka. Tunahitaji kwanza kujua ni kivipi tutafuzu MTN8. Hivyo nafasi 8 za juu ni lengo letu kubwa.”

Msimu wa kwanza Baroka kumaliza nafasi 2 za mwisho kabla ya kushinda mchezo wa mtoano kwenye mchezo wa kuamua timu ya kushuka daraja.

Msimu uliopita walitawala mechi za awali kabla ya kuporomoka mpaka nafasi ya 14.

Mshambuliaji hatari wa zamani wa Kaizer Chief, Wedson Nyirenda ametwaa mikoba ya kuinoa klabu hiyo.

Mashindano M G Y R Dkk
Jumla 32 3 3 2.853′
28 3 2 2.493′
3 1 270′
1 90′
Y-Njano, R-Nyekundu, Dkk-Dakika, G-Mabao, M-Mechi.

Banda alicheza michezo 28 kwa klabu hiyo. Kiwango chake ndani ya klabu yake, pamoja na kuitwa kwake timu ya taifa mara kwa mara kumefanya aanze kuwindwa na timu mbalimbi.

Kocha mkuu wa Mamelodi Pitso Mosimane anafahamu uwezo wa Banda vyema. Banda ndiye mchezaji bora ea Baroka msimu uliopita bila shaka. Baroka wana haki ya kumzuia lakini Mosimane pia anaweza kumshawishi Banda na kupata huduma zake. Kadi yake ya kwanza alipata dakika ya 59′ baada ya kunawa mpira kwenye mchezo dhidi yao na Kaizer Chiefs 1-0 Baroka FC ambapo katika mchezo pia alifunga bao lililoipatia Baroka sare.

Abdi Banda umri wake unamruhusu kwani amefikisha miaka 23 kwa mujibu wa transfermarket.com. inaonesha alizaliwa tarehe 20 mwezi Aprili 1993. Abdi Banda yupo chini ya wakala wa Siyavumi.

Hata hivyo klabu yao msimu imefanya usajili wa kutosha. Elvis Chipezeze, Tshediso Patjie, Bheki Maliba, Thabo Moseki, Bonginkosi Makume,Siseko Manana, Armand Gnanuillet, Ananias Gebhardt, Shabani Hussein, Shabani Hussein na Orebotse Mongae.

Klabu hiyo ya Baroka pia imekuwa unataratibu wa kutoa Mamiss. Shindano lao linajulikana kama Miss Baroka ili kuvutia zaidi mashabiki na kufanya uwekezaji. Simba na Yanga Vipi kuna uwezekano wa Miss kariakoo Derby???😀

Hata hivyo Abdi Banda alipewa tuzo ya kuwa mchezaji bora wa mwezi mei mwaka huu wa klabu ya Baroka. Pia Abdi Banda yupo nchini kwa ajili ua maandalizi ya harusi yake

Usiache kuzidi kutufuatilia kwenye kurasa zote za Shaffih dauda (Instagram na facebook) Pia dauda tv kwenye youtube.

Mimi ni Privaldinho (Instagram)

RC Mwanza kuwa wa kwanza kujisajili Rock City Marathon

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella anatarajiwa kupamba uzinduzi wa usajili wa mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa unaotarajiwa kuanza Septemba 1 katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu katika Uwanja vya CCM Kirumba  jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya Capitial Plus Internantional,  Bw. Zenno Ngowi, RC Mongella ndiye atakuwa wa kwanza kujisajili katika mbio hizo akiwakilisha wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga na  Simiyu.

“Zoezi hilo la usajili litaanza rasmi Septemba 1 katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo Igoma, Buzuruga, Airport Mwanza, Rock City Mall, Chuo Kikuu cha SAUT, Nyegezi Stand, Mwanza Hotel, Nyamagana Stadium, Dampo pamoja na Nyakato.

Alisema usajili huo pia utahusisha ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.

“Mwaka huu tumeongeza idadi ya vituo vya usajili wa mbio hizi lengo likiwa ni kuwafikia washiriki wengi zaidi ambapo pia kwa upande wa Dar es Salaam usajili utafanyika maeneo ya Mlimani City Vodashop, Vodacom Tower barabara ya Bagamoyo, Masaki Vodashop na Vodashop Arusha,’’ alisema.

Mbio hizo zinazolenga kutangaza Utalii wa Kanda ya Ziwa zimefanikiwa kuvutia wadhamini kadhaa wakiwemo kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper, Vodacom Tanzania, NMB, Tawa, Tanapa, TTB, NSSF, SDS, Gold Crest, New Mwanza Hotel, CF Hospital, CocaCola, Metro FM, EF Outdoor, Tonito , KK Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Link.

Aliongeza kuwa katika kurahisisha zaidi zoezi hilo, usajili wa mwaka huu pia utafanyika kwa njia ya simu kupitia huduma ya M-Pesa.

“Tupo kwenye hatua za mwisho kuhakikisha kwamba washiriki wa mbio hizo wanaweza kujisajili kupitia huduma ya M-PESA ili kuokoa muda na kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi na zaidi linahusisha eneo kubwa la nchi kwa kuwa huduma ya M-PESA inapatikana kila kona ya nchi,’’ alisema.

Alisema usajili huo utahusisha mbio za km 42 kwa wanaume na wanawake, Kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, km 5 kwa washiriki kutoka kwenye mashirika (Corporates) na walemavu wa ngozi, km 3 kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 55 na kuendelea pamoja na km 2.5 kwa watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 10.

Rotary Dar Marathon yaadhimisha miaka kumi ya kubadilisha maisha

$
0
0

Tukio maarufu la riadha la Rotary Dar Marathon ambalo hufanyika siku ya 14 Oktoba – siku ya Nyerere kila mwaka tangu 2009 litaadhimisha mwaka wa kumi tangu kuanza kwa tukio hilo. Dhima ya Rotary Dar Marathon inaendelea kuwa “ponya maisha, badilisha jamii” na ni katika mwaka wa tatu tangu RDM imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za hospitali ya (CCBRT) kuwa na mradi wa hsopitali binafsi ili waweze kupunguza gharama ya hudua za ulemavu zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wana jamii.  Fedha zote zitakazokusanywa mwaka huu kutokana na tukio la RDM zitakabidhiwa kwa CCBRT ili kukamilisha ujenzi wa kliniki hiyo binafsi na manunuzi ya vifaa husika.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Rotarian Catherinerose Barreto, alisema kwamba kamati inayojumuisha wajumbe kutoka klabu nane za Rotary za jijini Dar es Salaam imeshaanza maandalizi kuhakikisha mwaka huu RDM inakuwa tukio ambalo ni la ubora wa hali ya juu. Aliongeza pia mlezi wa RDM Mheshimiwa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi atakuwepo na kushiriki matembezi ya siku hiyo.

Mkuu wa kitengo cha ruti za Rotary Dar Marathon, Diamond Carvalho akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Mbio hizo zitajumuisha matembezi ya kifamilia ya kujifurahisha ya kilomita 5 na 9, mashindano ya riadha na baiskeli ya kilomita 21.1 na 42.2.

Tukio la Rotary Dar Marathon (RDM) licha ya kulenga lengo msingi la kuchangisha fedha kusaidia shughuli mbalimbali ili kuboresha ubora wa maisha kwa jamii zetu pia linahakikisha kutoa tukio lenye ubora wa kimataifa na la kufurahiwa na wanaoshiriki katika mbio au matembezi. Kila mwaka RDM inachukua hatua za ziada kuhakikisha tukio linafanyika katika kiwango cha juu ili washiriki wote ambao ni wanariadha wataalamu na wengineo wanafurahia siku hiyo na pia kuweza kutumia shindano kama njia ya kuongeza uzoefu wao na kukua katika michezo wa riadha.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Hawa Mkwela akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.

Mkuu wa njia za RDM Rotarian Diamond Carvallo, naye alisema kwamba anatarajia tukio la mwaka kuvutia washiriki ya zaidi 16,000, na baadhi pia inatarajiwa kuwa baadhi ya washiriki watakuja kutoka nje ya nchi. Katika tukio la RDM mwaka huu kutakuwa na mashinda ya riadha na baiskeli kwa kilomita 21.1km na 42.2  vilevile matembezi ya kujifurahisha ya kilomita  5 na 9. Riadha na matembezi yote yataanzia na kumalizika katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Gavana wa Rotary na mwenyekiti wa RDM, Sharmila Bhatt aliongeza, “ni sera yetu kufanya kazi kwa pamoja na mashirika mbalimbali katika juhudi zetu za kuleta mabadiliko katika katika jamii zetu. Tunaamini kwamba kufanya kazi pamoja kutaleta mafanikio makubwa katika jamii kwa ujumla. Tunapenda kuwashukuru Bank M kwa kushirikiana nasi kwa miaka tisa iliyopita na SBC – Pepsi kwa kuendelea na udhamini wao Tshirts,-vinywaji na mwaka huu kwa kuongeza msaada zaidi katika kufanikisha RDM. Mwaka huu tutakuwa washirika wapya na tunafurahi sana kuweza kuleta tukio la Rotary Dar Marathon mwaka huu hii ikiwa ni tukio letu la 10.”

Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon, Sharmila Bhatt akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Rotary Dar Marathon inatarajia kuwavutia washiriki 16,000 kwa mwaka huu.

Kwa miaka 9 iliyopita, Rotary Dar Marathon imeendeleza miradi kadhaa kama vile kupanda miti 27,000, kutoa vifaa vya maji na usafi wa mazingira kwa shule 27, kujenga wodi ya watoto ya saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia kukarabati na kuweka vifaa katika kituo cha ujasiriamali cha Rotary katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Viewing all 565 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>