Katumbi, 51, amekutwa na hatia ya kuuza jingo kinyume cha sheria huko Lumbumbashi ambako ni makao makuu ya biashara zake na ametozwa pia faini ya dola za kimarekani 6,000,000 sawa na shilingi bilioni 12 za kitanzania.
Inaamika kuwa anaungwa mono na vyama saba vya upinzani kwa ajili ya kumkabili Rais wa DRC Joseph Kabila katika uchaguzi wa rais ambao awali ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana lakini uchaguzi tayari umeahishwa na unatarajiwa kufanyika mwakani.
Rais Kabila yuko madarakani tangu mwaka 2001 alipoingia madarakani baada ya kifo cha baba yake Laurent Kabila.
Mahakama imechukua uamuzi huo wakati huu ambapo klabu yake ya TP Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika mwaka 2015 wakijiandaa kuja Tanzania kukabiliana na Yanga kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Afrika hatua ya makundi mchezo unaotarajia klupigwa Jumanne ijayo June 28 kwenye uwanja wa taifa.