Kama kawaida kwenye Ndondo Cup ndiyo ilipo burudani ya soka kwasasa ‘kibongobongo’ Ulaya wao wana michuano yao ya Euro wati bara la America wao wao wanazungumza habari za Copa America.
Sio siri upekee wa michuano ya Ndondo Cup uko nje ya uwanja, mashabiki wa timu mbalimbali hujitokeza kuzi-support timu zao kwa style tofauti kila kukicha kitu ambacho kinawavutia watazamaji wa michuano hii.
Leo mashabiki waliouteka uwanja wa Bandari ni wa timu ya Keko Furniture pale wakati inacheza dhidi ya Tabata United mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2.
shaffihdauda.co.tz kama kawaida haikufanyi uwe nyuma, imekukusanyia picha hizi za matukio mbalimbali yaliyojiri uwanjani.