Sports Etra Ndondo Cup imeendelea tena leo kwenye viwanja viwili tofauti jijini Dar ikiwa ni hatua ya makundi.
Kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii zamani uwanja wa Bandari, Temeke Market wameichapa Kinondoni FC mabao 2-1. Mabao yote ya Temeke Market yakiwekwa kambani na Uhuru Selemani wakati bao la Kinondoni FC likifungwa na Vicent Costa.
Brian yeye ni nahodha wa timu ya Temeke Market ambaye hajasita kuisifia michuano ya Ndondo Cup lakini akianza kwa kuzungumzia mchezo wao dhidi ya Kinondoni FC.
“Mechi ya leo ilikuwa ni nzuri, ngumu na yenye ushindani vijana wameonesha uwezo lakini timu yetu ilikuwa bora kuliko Kinondoni FC. Mpaka sasa tunapointi saba tukiwa tunaongoza kundi letu”.
“Ndondo Cup ni mashindano mazuri, kwanza yanaleta msisimko kwa vijana wanaotaka kucheza na kuonesha uwezo lakini kuna wachezaji wenye majina kubwa kwenye soka la Tanzania ambao wanatupa changamoto sisi vijana na haya mashindano yanaonekana yanatija”.