Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

 KILIMANJARO FC TIMU YA WATANZANIA INAYOCHEZA LIGI SWEDEN, LENGO NI KUWATOA WABONGO

$
0
0

Kilimanjaro 1

Na Baraka Mbolembole

Goerge Kusila ni mwenyekiti, Humphrey J. Mwigama ni makamu mwenyeki pia ni kocha, Andrey Eustace ni katibu mkuu, Nyupi Mwakikosa ni meneja, Suleimani K. Said ni mratibu na Amon Gyunda ni mweka hazina.

Watu hawa 6 niliotaja majina yao pamoja na wachezaji maarufu wa zamani wa Tanzania kama Shekhan Rashid, Athumani Machuppa na Watanzania wengine wapenda kandanda wameamua kufanya kitu kikubwa wakiwa nchi ya ng’ambo, tena barani Ulaya kuanzisha timu ya kandanda ambayo lengo lake kubwa ni kuvisaidia vipaji vichanga kutoka Tanzania na nchini nyingine barani Afrika kucheza mpira wa kulipwa barani Ulaya.

Kilimanjaro FC ndiyo jina la klabu ninayoizungumzia hapa.

Kilimanjaro

“Kilimanjaro FC nia yetu kubwa ni kuifikisha daraja la juu ‘i mean’ daraja la pili ili tuweze kuwasaidia watanzania wenzetu kuja kucheza huku na kuonekana na kuuzwa kwenye timu nyingine. Zaidi  kwa sasa bado tuna nguvu kidogo, tunataka kuisogeza kidogo na tukiacha kucheza tutakuwa kama viongozi ili tuweze kufanikisha malengo yetu”

Anasema Shekhan Rashid mchezaji wa timu hiyo ambaye pia amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania na vilabu ya Singida United, Simba SC, Mtibwa Sugar, na Azam FC wakati nilipofanya naye mahojiano marefu akiwa nchini Sweden.

Katika nchi ya Sweden kuanzia ligi daraja la 7 (daraja la mwisho kabisa ambalo Kilimanjaro FC wanacheza) hadi ligi daraja la tatu huwa ni ligi za ridhaa-yaani si za kulipwa. Kuanzia ligi daraja la pili huwa ni ligi za kulipwa na lengo kubwa la Watanzania hao ni kuifikisha timu hiyo katika madaraja ya juu zaidi.

“Huku (Sweden) kuanzia daraja la Pili ni profesional mnaweza kuleta wachezaji kutoka nje hivyo malengo yetu ni kuweza kuifikisha huko ili tuweze kuleta wachezaji kutoka kwetu Tanzania waje na kuicheza FC Kilimanjaro ili timu zikiwaona zikiwataka tunawauza tunaleta wengine ili tuwe na wachezaji wengi wa kulipwa kutoka Tanzania.”

Kilimanjaro 3

“Kutoka daraja  la saba mpaka kufika la pili sio ngumu sana. Sisi wote tulifikiria wazo hilo maana itakuwa ni njia moja wapo rahisi kwa watanzania wenzetu walioko tanzania kuja kucheza mpira huku kiurahisi. Na inawezekana maana huku kuna timu za waraabu kutoka Syria zipo kibao madaraja la kwanza, la Pili , la Tatu,  mpaka la Nne.”

Kilimanjaro FC katika msimamo wa ligi daraja la 7 hadi kufikia game ya raundi ya 7 ilikuwa nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na alama 16 baada ya kushinda game 5 sare moja na kupoteza mechi moja. Solna FC inaongoza kwa alama tatu zaidi katika ligi hiyo yenye timu kumi.

Kilimanjaro 2

”Tuna uongozi mzuri tu na tunapata support kubwa kutoka ubalozi wetu wa Tanzania hapa. Kuna wachezaji Watanzania wengi na Wakenya kama wanne tu na kipa ni Mgambia. Asilimia kubwa ni Wabongo tu.”

“Kwa sasa tupo katika nafasi ya pili baada ya kucheza game 7 na Oktoba 8 ndiyo ligi inatamalizika na timu moja itapanda, anaengoza ndiyo tunamaliza nae mechi ya mwisho. Hata asipofungwa sisi tutampiga tu.”

www.shaffihdauda.co.tz inawapongeza wanadinga hao wa zamani waliotamba nchini kwa wazo lao makini, tutawaunga mkono siku zote.

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>