Azam FC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa Kundi B michuano ya Mazpinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.
Goli pekee katika mchezo huo limefungwa na Shabani Idd dakika ya 76 kipindi cha pili baada ya kufanikiwa kumpita golikipa wa Zimamoto kisha kufunga bao hili kiulani.
Mchezo kati ya Azam vs Zimamoto ulianza saa 10:00 ikiwa ni mchezo wa kwanza wa Kundi A wakati mchezo mwingine wa kundi hilo utaikutanisha Yanga dhidi ya Jamhuri kuanzia saa 2:15 usiku.
Ushindi wa leo ni wa pili kwa Azam FC bila makocha wao wakihispania ambao walitimuliwa juma lililopita. Ushindi wa kwanza kwa Azam bila makocha hao ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons.
Kwa sasa Azam ipo chini ya kocha wa timu ya vijana wa U-20 Idd Cheche ambaye anaisimamia kwa muda wakati mchakato wa kusaka kocha mkuu unaendelea.