Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Simba bingwa ligi ya U-20

$
0
0

simba-mtoto-2

Timu ya vijana ya Simba SC U-20 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la ligi kuu Tanzania bara kwa kuifunga Azam FC U-20 kwa mikwaju ya penati 5-3.

simba-mtoto-1

Mchezo wa fainali ulichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:00 usiku umeamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu zote kutoka sare ya kufungana magoli 2-2 ndani ya dakika 120.

simba-mtoto-3

Simba ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao katika mchezo huo, goli likifungwa dakika ya 14 kipindi cha kwanza lakini Azam wakasawazisha dakika 32 kupitia kwa Shaaban Idd aliyeunganisha pasi ya Odasi.

simba-mtoto-4

Said Issa akaifungia Azam bao la pili dakika ya 56 kipindi cha pili lakini dakika tano kabla ya mpira kumalizika, Simba wakasawazisha goli hilo.

Dakika 30 zikaongezwa kwa mujibu wa kanuni za mashindano na kufanya mchezo huo uchezwe kwa jumla ya dakika 120 ili kumpata mshindi.

simba-mtoto-5

Dakika 30 za nyoingeza zikaisha bila mshindi kupatikana na ndipo sheria ya mikwaju ya penati ikatumika ili kumpata bingwa.

Simba wakashinda kwa kufunga penati zao zote huku Azam wao wakikosa penati tatu na kuwaacha Simba wakitangazwa mabingwa wa ligi ya vijana 2016-17.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Latest Images

Trending Articles



Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>