Baada ya Temeke Market kubuka mabingwa wa Ndondo Cup 2016 kwa kuifunga Kauzu FC magoli 3-1, Shabani Kisiga ‘Malone’ alitangazwa mchezaji bora wa mechi hiyo lakini pia mchezaji bora wa mashindano ya Ndondo Cup kwa msimu huu.
Kisiga ametangazwa mchezaji bora wa mashindano na kocha Kenny Mwaisabula Mzazi ambaye ndiye alikuwa akiongoza jopo la kuwapata washindi wa tuzo za mchezaji binafsi katika mashindano ya msimu huu.
shaffihdauda.co.tz ikapata fursa ya kuzungumza na mchezaji bora Shabani Kisiga, na haya ndiyo aliyoyasema: “Namshukuru Mungu lakini pia najisikia furaha, bado malengo yangu ni kucheza professional footbal kwasababu hapa Tanzania ni kama najiandaa, lengo langu ni kucheza nje na ninaimani nitafika kwasababu bado sijakata tamaa.”
Nyota huyo wa mchezo wa leo amekabidhiwa amekabidhiwa kiasi cha shilindi 50,000 kama ilivyokawaida ya mashindano kwenye msimu huu ambapo kila mechi kuanzia hatua ya mtoano (16 bora) kulikuwa na zawadi kwa mchezaji bora wa kila mchezo ambaye amekuwa akizawadiwa shilingi 50,000, T-shirt na flana kutoka gatezi la Mwanaspoti.
Kutokana na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mahindano, Kisiga amejishindia kitita cha shilingi 1,000,000 (milioni moja) za Tanzania lakini pia amepewa king’amuzi cha Azam TV, pea moja ya viatu vya kuchezea mpira pamoja na mpira mmoja.