Quantcast
Channel: NYINGINE – ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Costal Union imerejea VPL, kocha kaweka historia baada ya miaka 30

$
0
0

Hatimaye Costal Union ya Tanga imefanikiwa kurejea ligi kuu Tanzania bara kwa ajili ya msimu ujao (2018/19) baada ya kupata matokeo ya ushindi wa magoli 2-0 dhiodi ya Mawenzi market ya Morogoro kwenye mchezo wa kundi b ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kocha mkuu wa Costal Union juma mgunda na msaidizi wake Joseph Lazaro wameandika rekodi ya aina yake kwa kuwa ndio wachezaji walioipa ubingwa timu hiyo miaka 30 iliyopita wakiwa wachezaji leo wakiwa makocha wanaiwezesha kupand daraja kucheza ligi kuu.

“Mwaka 1988 mimi na msaidizi wangu Joseph Lazaro tulikuwa wachezaji wa Costal Union tulioipa ubingwa Coastal Union mwaka huo, leo mimi tena nikiwa na mwenzangu yuleyule (Joseph Lazaro) baada ya miaka 30 tunatengeneza historia nyingine. Ni jambo linalonifurahisha sana na litachukua muda mrefu kufutika kwenye kumbukumbu zangu,” Juma Mgunda.

“Umati wa mashabiki uliokuja leo uwanja wa Jamhuri Morogoro kuishangilia timu yao ili ipande daraja, unanikumbusha enzi zetu wakati tunacheza tunapata support kubwa kutoka kwa mashabiki kama hivi, ni jambo la kufurahisha linalonikumbusha mbali na kunijengea historia nyingine kwenye timu ya Coastal Union.”

Magoli ya Coastal Union katika mchezo huo yamefungwa na Raidhin Hafidh na mkongwe Athumani Idd ‘Chuji’ nyota wa zamani wa polisi Dodoma, Simba, Yanga, Mwadui pamoja na timu ya taifa ya tanzania ‘Taifa Stars’.

Kutoka Kundi B Costal na KMC zimefuzu kucheza ligi kuu Tanzania bara zikiungana na JKT Tanzania.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 565

Latest Images

Trending Articles



Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>