Shirikisho la masumbwi ya kulipwa nchini TPBC limeahidi kuendelea kutoa elimu kwa mabondia ambao bado hawafahamu utaratibu wa safari za kutoka nje ya nchi.
Rais wa TPBC Palasa Chaurembo amesema kutokana na mzozo ulioibuka kati yao na bondia Franciss Cheka kufuatia safari yake ya kuelekea nchini India kwa ajili ya pambano la kuwani ubingwa wa WBO, wameona ipo haja ya kutoa elimu ili kuepusha malumbano yasiyo na lazima.
“Tuanaendelea kuwapa elimu kupitia makundi lakini pia tutaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari lakini baraza linampango wa kuwaita wanamichezo wote kwasababu kuna sitofaham kwa wale waliokuwa wanafanya kazi kiholela, sasahivi vitu vinatakiwa viende kwa kufata mstari, walikuwa wanawadangaya mabondia kwa hiyo inakuwa ngumu sana mabondia kuelewa.”
“Ngumi ni mchezo hatarishi inatakiwa mabondia walinde afya zao bila kuangalia pesa tu, tukiwa na chama cha ngumi kinachojitambua, kitasimamia vizuri afya za wachezaji na maslahi ya mabondia. Nawashauri mabondia wasikilize ushauri wa serikali pamoja na chama cha masumbwi TPBC ili waishi kwa muda mrefu katika masumbwi.”