Timu ya Temeke Market imefanikiwa kutangulia fainali ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup 2016 baada ya kuifunga Makumba FC kwenye kwa penati 3-1.
Dakika 90 za pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Bandari Tandika lilimalizika kwa suluhu (0-0) na kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano ilibidi mshindi aamuliwe kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Ushindi huo unaifanya Temeke Market ikutane na mshindi wa nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Misosi FC dhidi ya Kauzu FC.
Michuano ya Ndondo Cup inapewa nguvu na Dr. Mwaka chini ya kampuni yake ya Foreplan, Azam TV pamoja na gazeti la Mwanaspoti.